Siku ya Kuripoti Chuo cha Polisi Moshi 2025 kwa Vijana Waliochaguliwa

Siku ya Kuripoti Chuo cha Polisi Moshi 2025 kwa Vijana Waliochaguliwa

Jeshi la Polisi Tanzania limewatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kipolisi kwamba wanatakiwa kuripoti katika Shule ya Polisi Moshi kati ya tarehe 12 hadi 14 Juni 2025, kwa ajili ya kuanza rasmi mafunzo yao. Taarifa hiyo imetolewa rasmi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camilius Wambura, mnamo Jumapili, Juni 1, 2025, ambapo aliwataka vijana wote waliofaulu mchakato wa usaili uliotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania kufuata utaratibu uliowekwa kwa ajili ya kuripoti.

Siku ya Kuripoti Chuo cha Polisi Moshi 2025 kwa Vijana Waliochaguliwa

Taratibu za Kuripoti kwa Makundi Mbalimbali ya Vijana

1. Waliofanyiwa Usaili Dar es Salaam (Makao Makuu ya Polisi)

Kwa wale waliohudhuria usaili katika vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam, wanatakiwa kuripoti katika uwanja wa gwaride, Kambi ya Polisi – Barabara ya Kilwa.

  • Tarehe ya kuripoti: Juni 12, 2025
  • Muda wa kuripoti: Saa 12:00 asubuhi
  • Lengo: Kuungana kwa pamoja kwa ajili ya kusafiri kuelekea Shule ya Polisi Moshi.

2. Waliofanyiwa Usaili katika Mikoa ya Tanzania Bara

Vijana waliopitia usaili katika mikoa mingine ya Tanzania Bara (nje ya Dar es Salaam) wanapaswa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa waliyofanyia usaili.

  • Tarehe ya kuripoti: Juni 11, 2025
  • Muda wa kuripoti: Saa 2:00 asubuhi
  • Lengo: Kupata utaratibu wa safari ya pamoja kuelekea Moshi.

3. Waliofanyiwa Usaili Zanzibar (Unguja na Pemba)

Kwa upande wa vijana waliopitia usaili visiwani Zanzibar (Unguja na Pemba), wanapaswa kuripoti katika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya safari.

  • Tarehe ya kuripoti: Juni 11, 2025
  • Muda wa kuripoti: Saa 2:00 asubuhi
  • Lengo: Kupangiwa utaratibu wa safari ya kuelekea Shule ya Polisi Moshi.

Jeshi la Polisi limewasihi vijana wote waliochaguliwa kufuata kwa makini maagizo yaliyotolewa, kuheshimu muda wa kuripoti na kujiandaa vyema kwa safari ya kuanza maisha mapya ya mafunzo ya kijeshi.

Hii ni nafasi ya kipekee kwa vijana kujifunza, kuimarika kitaaluma na kuwa sehemu ya chombo muhimu cha ulinzi na usalama wa Taifa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fiston Mayele Ndie Mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2024/2025
  2. Wafungaji Bora Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
  3. Washindi Tuzo Za Baraza La Michezo Tanzania BMT 2024
  4. Pyramids Yabeba Ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika 2024/2025 kwa Mara ya Kwanza Kihistoria
  5. Wachezaji wa Simba Walioitwa Kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa June 2025
  6. Hawa Apa Maofisa wa Mechi ya Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
  7. Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa kambini Kuelekea COSAFA na Mechi ya Kirafiki
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo