Simba SC Kufanya Maamuzi Magumu Kuhusu Hatma ya Kipa Wao

Simba SC Kufanya Maamuzi Magumu Kuhusu Hatma ya Kipa Wao

Dar es Salaam, Ijumaa – Mabosi wa Simba SC leo wanatarajiwa kukutana mezani kwa kikao kizito kinacholenga kumaliza utata wa muda mrefu kuhusu hatma ya mmoja wa makipa wao waliokuwa wakihudumu kikosini.

Taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa mchakato wa kumtoa kipa huyo kwa mkopo umekwama baada ya mchezaji mwenyewe kugomea pendekezo hilo na kusisitiza kuvunja mkataba wake rasmi ili alipwe stahiki zake na kuondoka kabisa Msimbazi.

Simba SC Kufanya Maamuzi Magumu Kuhusu Hatma ya Kipa Wao

Simba SC Kwenye Mshikemshike

Kwa mujibu wa duru za ndani, Simba SC ilipanga awali kumpeleka kipa huyo kwa mkopo Namungo FC, lakini mpango huo uliporomoka baada ya mchezaji kuonyesha kutokuwa tayari kukubali suluhu hiyo. Aidha, kulikuwa pia na wazo la kumtuma JKT Tanzania, lakini mpango huo pia ulifutika baada ya JKT kumchukua kipa Ramadhan Chalamanda kutoka Kagera Sugar.

Hali hii imeibua mjadala mkubwa ndani ya uongozi wa Simba, ambao sasa unalazimika kufanya maamuzi magumu kwa kuangalia namna bora ya kumaliza suala hili bila kuathiri jina la klabu na hadhi ya mchezaji husika.

Historia Fupi ya Kipa Huyo

Kipa huyo, aliyezaliwa Aprili 19, 2000 huko Pemba, Zanzibar, bado ana mkataba wa miaka mitatu na Simba baada ya awali kusaini mkataba wa miaka mitano. Hata hivyo, ameitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili pekee, na kwa msimu mpya wa 2025/2026 hakuwa sehemu ya mipango ya benchi la ufundi.

Simba SC tayari imejihakikishia huduma za mlinda mlango mpya, Yakoub Suleiman kutoka JKT Tanzania, jambo lililoonyesha wazi kuwa nafasi ya kipa huyu haipo tena kwenye ramani ya kikosi cha kwanza.

Hatua Zilizochukuliwa na Simba SC

Chanzo cha karibu na Simba SC kimeeleza kuwa uongozi unataka kumaliza suala hili kwa amani ili kumpa mchezaji nafasi ya kutafuta changamoto mpya katika taaluma yake. Klabu inatambua kuwa kipa huyo ameipitia ngazi zote tangu kikosi B, na hivyo anastahili heshima katika namna anavyotoka.

“Mchezaji ameonyesha wazi hataki tena mpango wa mkopo. Simba sasa inatafuta njia sahihi ya kuvunja mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote mbili,” kilieleza chanzo hicho.

Taarifa zaidi zinadai kuwa huenda kipa huyo akatua Tabora United, klabu ambayo tayari ilikuwa kwenye mazungumzo naye. Hata hivyo, dili hilo lilikwama kutokana na kikwazo cha mkataba wake na Simba. Endapo mchakato wa kuvunja mkataba utamalizika rasmi, Tabora United inaweza kuwa kituo kipya cha kipa huyo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Makundi ya CECAFA Kagame Cup 2025
  2. Mechi ya Pili ya Dabi ya Kariakoo Simba vs Yanga Kuchezwa Desemba 13 2025
  3. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026
  4. Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 Kuanza September 17 2025
  5. Simba Yamtambulisha Selemani Mwalimu Kutoka Wydad AC kwa Mkopo wa Mwaka
  6. Simba Kuivaa Gor Mahia ya Kenya Kwenye Kilele cha Simba Day
  7. Mshambuliaji Clement Mzize Asaini Kuendelea na Yanga Hadi 2027
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo