Simba VS Es Tunis Leo 1/02/2026 Saa Ngapi
Dar es Salaam. Leo jioni saa 10:00, klabu ya Simba SC itakuwa na kibarua kizito katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwakaribisha Esperance de Tunis kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi itakayokuwa na umuhimu mkubwa kwa hatima ya Simba kwenye mashindano hayo. Mechi hiyo itarushwa mubashara kupitia AzamSports1HD, huku Simba ikihitaji ushindi wa lazima ili kuendelea kubaki kwenye mbio za kufuzu hatua ya robo fainali.
Taarifa Kamili Kuhusu Mchezo wa Simba VS Es Tunis Leo 1/02/2026
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mechi | Simba vs ES Tunis |
| Tarehe | 1 Februari 2026 |
| Saa | 10:00 jioni |
| Uwanja | Benjamin Mkapa |
| Matangazo | AzamSports1HD |
| Matokeo ya awali | ES Tunis 1–0 Simba |
Simba Katika Presha ya Ushindi
Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa katika nafasi ngumu, kwani matokeo yoyote tofauti na ushindi yatamaanisha safari yao katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu inafikia tamati. Ushindi wa leo pekee ndio utakaowapa matumaini ya kuendelea kupigania nafasi ya kusonga mbele, ingawa bado italazimika kushinda mechi mbili zilizosalia na kutegemea matokeo ya timu nyingine kwenye kundi lao yawe ya manufaa.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumamosi, Januari 24, 2026, Simba ilipoteza kwa bao 1-0 ugenini dhidi ya Esperance, jambo linaloifanya mechi ya leo kuwa ya kulipiza kisasi na kurejesha matumaini.
Waamuzi Kutoka Msumbiji
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Msumbiji, wakiongozwa na refa Celso Alvacao, akisaidiwa na Zacarias Baloi na Venestancio Cossa, huku mwamuzi wa nne akiwa ni Simoes Guambe.
Nguvu Mpya Ndani ya Kikosi cha Simba
Simba imeingia katika mechi hii ikiwa na nguvu mpya baada ya kuwasajili wachezaji sita wa kigeni katika dirisha dogo la usajili. Wachezaji hao ni Jospin Loemba, Libasse Gueye, Anicet Oura, Clatous Chama, Djibrilla Kassali na Ismael Toure, ambao wanatajwa kuongeza ushindani na ubora ndani ya kikosi cha kocha Steve Barker.
Kauli ya Kocha Barker
Akizungumzia mechi hiyo, kocha wa Simba Steve Barker alisema msimamo wa kundi lao unawalazimisha kupata ushindi.
“Tunajua kwamba tunacheza dhidi ya timu nzuri. Tunaamini kwamba bado nafasi yetu ipo ya kusonga mbele ukizingatia tutakuwa nyumbani na tutakuwa na sapoti ya mashabiki wetu,” alisema Barker.
Aliongeza kuwa Simba inapaswa kuboresha matumizi ya nafasi.
“Ili tupate ushindi tunatakiwa kuimarika hasa katika kutumia nafasi. Tunatakiwa kutengeneza sana nafasi na tunafahamu kwamba katika Ligi ya Mabingwa Afrika huwa hakuna timu rahisi.”
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply