Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?

Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?

Mnyama Simba SC leo anashuka dimbani kuwakaribisha walima sukari wa Kagera Sugar katika mchezo wa kuamua uhai wa ndoto yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025. Mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa wekundu wa Msimbazi ambao wanalazimika kushinda ili kuendelea kubaki kwenye kinyang’anyiro cha taji, kabla ya kukamilisha msimu dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Juni 25.

Simba SC kwa sasa wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, wakiwa na pointi 75, wakizidiwa kwa pointi moja tu na Yanga SC ambao wana pointi 76. Ushindi katika mchezo wa leo utairudisha Simba kileleni, ingawa kwa muda, na kuweka shinikizo kubwa kwa Yanga kuelekea mechi ya mwisho ya msimu.

Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025 Saa Ngapi na Wapi Utachezwa?

Mchezo huu muhimu utafanyika leo, Jumamosi tarehe 22 Juni 2025, saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).

Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?

Simba inajivunia kikosi kipana chenye wachezaji wazoefu wa mechi kubwa, na wanatambua wazi kuwa kushindwa leo kunaweza kumaliza ndoto yao ya ubingwa kabla hata ya kumenyana na Yanga. Kwa mantiki hiyo, kocha na benchi lake la ufundi wanatarajiwa kuanza na kikosi bora, kikilenga kupata mabao ya mapema ili kuweka presha kwa wapinzani wao.

Kwa upande wa Kagera Sugar, licha ya kuwa hawapo kwenye mbio za ubingwa, ni timu yenye historia ya kusumbua vigogo na haitakuwa rahisi kwa Simba kuibuka na ushindi bila mapambano ya kweli.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tanzania Yashinda Ubingwa wa CECAFA Wanawake 2025 Kupitia Twiga Stars
  2. KMKM Mabingwa wa FA Cup Zanzibar 2025 Baada ya Ushindi wa 4-2 Dhidi ya Chipukizi
  3. Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
  4. Klabu ya Liverpool Yamwaga Mamilioni Kumnasa Florian Wirtz
  5. Viingilio Simba SC vs Kagera Sugar 22/06/2025
  6. Viingilio Yanga VS Dodoma Jiji 22/06/2025
  7. Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
  8. Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo