Simba Yamtambulisha Selemani Mwalimu Kutoka Wydad AC kwa Mkopo wa Mwaka

Simba Yamtambulisha Selemani Mwalimu Kutoka Wydad AC kwa Mkopo wa Mwaka

Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi mshambuliaji Selemani Mwalimu kutokea klabu ya Wydad Athletic Club (Wydad AC) ya nchini Morocco kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja. Hatua hii inamwezesha mchezaji huyo kurejea tena kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, miezi kadhaa tu baada ya kuondoka katika dirisha dogo la usajili msimu uliopita kuelekea Wydad.

Simba Yamtambulisha Selemani Mwalimu Kutoka Wydad AC kwa Mkopo wa Mwaka

Mwalimu amekuwa sehemu ya wachezaji wakitanzania waliopata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa, ikiwemo Kombe la Dunia la Klabu, jambo linaloongeza uzoefu wake ndani ya kikosi kipya cha Simba. Ujio wake unatarajiwa kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ya wekundu wa Msimbazi, ambayo imekuwa ikihitaji nyongeza ya nguvu na ubunifu zaidi kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, usajili wa Selemani Mwalimu ni kwa mkopo wa mwaka mmoja pekee, bila kuwepo kwa kipengele cha Simba kumnunua moja kwa moja kutoka Wydad AC. Hii inamaanisha kuwa mchezaji ataendelea kuwa mali ya Wydad, huku akitumikia Simba kwa muda wote wa msimu ujao.

Hata hivyo, uwepo wake katika kikosi cha wekundu wa Msimbazi unachukuliwa kama suluhisho la muda mfupi linaloweza kuleta matokeo makubwa, hasa kutokana na uwezo wake wa kucheza katika nafasi tofauti za ushambuliaji na uzoefu alioupata kimataifa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mshambuliaji Clement Mzize Asaini Kuendelea na Yanga Hadi 2027
  2. Opah Clement Atambulishwa Rasmi SD Eibar ya Hispania
  3. Yanga SC Kucheza Dhidi ya Bandari FC Siku ya Wiki ya Mwananchi
  4. Morocco Yatinga Fainali ya CHAN Baada ya Kuifunga Senegal kwa Penalti
  5. Madagascar Kukipiga Dhidi ya Morocco Fainali ya CHAN 2025
  6. Simba SC Yasogeza Tarehe ya Uzinduzi wa Jezi Mpya 2025/2026
  7. Viingilio Simba Day 2025
  8. Ligi Kuu Zanzibar ZPL 2025/2026 kuanza Septemba 20
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo