Simba Yatangaza Bei ya Jezi Zao Mpya za 2025-2026

Simba Yatangaza Bei ya Jezi Zao Mpya za 2025-2026

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wametangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya pre-order kwa jezi mpya watakazovaa katika msimu wa 2025/2026. Tangazo hili limekuja kupitia kampuni mshirika wa mauzo ya jezi, Jayrutty Investment East Africa Ltd, ambapo mpango huu maalum unalenga wafanyabiashara wanaonunua jezi kwa bei ya jumla.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei ya jumla kwa jezi mpya za Simba SC imetajwa kuwa TZS 32,000 kwa pisi moja, na utaratibu huu wa awali wa kuagiza unafunguliwa ili kuruhusu wafanyabiashara kujipanga mapema kabla ya uzinduzi rasmi wa jezi hizo.

Masharti ya Ununuzi wa Bei ya Jumla

Jayrutty Investment East Africa Ltd imeweka sharti kwamba bei ya jumla itaanza kutumika kwa wateja watakaonunua bando tatu zenye rangi tatu tofauti. Kila bando moja lina jumla ya pisi 600, hivyo ununuzi wa bei ya jumla unalenga hasa wauzaji wakubwa wanaoweza kusambaza bidhaa kwa wingi.

Kampuni imehimiza wateja kulipia mizigo yao mapema ili kuepuka usumbufu au ucheleweshaji wakati wa uzinduzi wa jezi mpya. Hatua hii pia inawapa wafanyabiashara nafasi ya kuwa miongoni mwa wa kwanza kupata jezi hizo mpya, ambazo zinatarajiwa kuvutia mashabiki wengi wa Simba SC msimu ujao.

Simba Yatangaza Bei ya Jezi Zao Mpya za 2025-2026

Mawasiliano kwa Maelezo Zaidi

Kwa wafanyabiashara au wadau wa michezo wanaotaka kuweka oda zao mapema, timu ya mauzo ya Jayrutty Investment East Africa Ltd imeweka namba maalum za mawasiliano:

  • 📞 0675 666 333
  • 📞 0794 160 000
  • 📞 0690 255 540

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Makundi CHAN 2025
  2. Ratiba ya Mechi za Leo 12/08/2025 CHAN
  3. Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026
  4. Yanga Kucheza Mechi ya Kirafiki Dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda 15/08/2025
  5. Everton na Man City Wakubaliana Kuhusu Uhamisho wa Mkopo wa Grealish
  6. Wachezaji Wapya wa Yanga 2025/2026
  7. Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking 2025)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo