Taifa Stars Yaaga COSAFA Cup Licha ya Kuifunga Eswatini 2-1

Taifa Stars Yaaga COSAFA Cup Licha ya Kuifunga Eswatini 2-1

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, imeondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Eswatini katika mchezo wa mwisho wa Kundi C wa Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) 2025, uliopigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Toyota Free State, Bloemfontein, Afrika Kusini.

Licha ya ushindi huo wa kujivunia, Taifa Stars ilikuwa tayari imeondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kupoteza mchezo wao wa pili dhidi ya Madagascar siku ya Jumamosi. Hivyo basi, mchezo dhidi ya Eswatini ulikuwa wa heshima na kujipatia pointi za kufuta machungu.

Mchezo huo haukuwa rahisi kwa kikosi cha Tanzania kwani walijikuta wakitanguliwa kwa bao dakika ya 29 baada ya nyota wa Eswatini, Andy Junior Magagula, kufunga bao lake la pili katika mashindano haya.

Hata hivyo, wachezaji wa Taifa Stars hawakukatishwa tamaa. Waliongeza juhudi na kusawazisha dakika ya 37 kupitia kwa winga wa Azam FC, Iddi Suleiman ‘Nado’, aliyeonyesha ubora mkubwa katika mchezo huo.

Kwa kuwa walihitaji ushindi ili kuipita Madagascar kileleni mwa Kundi C, Eswatini walikuwa na presha kubwa ya kutafuta mabao zaidi kipindi cha pili. Lakini matumaini yao yalififia kabisa dakika ya 69, baada ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Shekhani Khamis, kufunga bao la ushindi kwa Taifa Stars kwa shuti dhaifu lililopenya mikononi mwa kipa wa Eswatini, Bongiswa Dlamini.

Matokeo hayo yameifanya Tanzania kumaliza katika nafasi ya pili ya Kundi C kwa pointi tatu, nyuma ya vinara Madagascar waliomaliza na pointi nne. Eswatini, waliomaliza na pointi moja, wanaungana na Taifa Stars kurejea nyumbani huku Madagascar wakisonga mbele.

Taifa Stars Yaaga COSAFA Cup Licha ya Kuifunga Eswatini 2-1

Hatua ya Nusu Fainali COSAFA Cup 2025

Kwa sasa, timu nne zimefuzu hatua ya nusu fainali ya COSAFA Cup 2025. Zinafanya maandalizi ya kupambana kwenye Uwanja huo huo wa Toyota Free State mnamo Juni 13 kama ifuatavyo:

  • Angola vs Madagascar – Saa 9:00 Alasiri
  • Afrika Kusini vs Comoro – Saa 12:00 Jioni

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Chelsea Yathibitisha Kumsajili Beki Mamadou Sarr Kutoka Strasbourg
  2. Yanga Kususia Fainali CRDB FA Cup Kisa Madeni ya Msimu Uliopita
  3. Yanga Yaibua Mambo Mapya Wakizungumzia Sakata la Dabi
  4. Matokeo Afrika Kusini vs Taifa Stars Leo 06/06/2025
  5. Afrika Kusini vs Taifa Stars Leo 06/06/2025 Saa Ngapi?
  6. Herry Sasii Afungiwa Soka Miezi 6 Kisa Mechi ya Simba na Singida
  7. Seif Karihe Acharazwa Faini na Kufungiwa Michezo Mitatu kwa Kurusha Chupa
  8. Tijjani Reijnders Asaini Manchester City Miaka Mitano Akitokea AC Milan
  9. Serikali Yajieka Pembeni na Sakata la dabi, yawaachia TFF
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo