Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Djigui Diarra Warejea Mazoezini
Baada ya kuwepo uvumi wa nyota wa Yanga Sc Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Djigui Diarra kuondoka klabuni huku baadhi ya mashabiki wakiamini kua wachezaji hao wameomba kuachana na kikosi baada ya kuto onekana katika kambi ya Yanga.
Kikosi cha Yanga kiliripoti Avic Town, Kigamboni, Dar es Salaam ambapo timu hiyo imeeka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2024/2025. Katika picha na video ambazo timu ya Yanga imekua ikitoa kuonesha wachezaji waliopo kambini katika mazoezi ya awali, mashabiki wengi walikua wakishangazwa na kuto onekana kwa Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Djigui Diarra ambao wote walikua na mchango mkubwa katika mafanikio ya klabu kwenye msimu wa 2023/2024.
Kuto onekana kwa nyota hao mazoezini kulizua tetesi za kua wachezaji hao wameomba kuachana na Yanga na wapo kwenye mazungumzo ya kujiunga na vilabu vingine jambo ambalo sasa limeonekana kua kutokua na ukweli wowote baada ya nyota hao kurejea rasmi nchni na wameingia kambini kuungana na wenzao kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa 2024-2025.
Tazama Video Ikionesha Mapokezi ya Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Djigui Diarra
🚨 Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Djigui Diarra wamerejea nchini na moja kwa moja wameingia kambini kuungana na wenzao kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa 2024-2025. pic.twitter.com/dRD9jD3bDY
— SportsArenaTz (@SportsarenatzTz) July 15, 2024
Mapendekezo ya mhariri:
- Stephane Aziz Ki Asaini Mkataba Mpya na Yanga SC
- Mishahara ya Wachezaji wa Yanga sc 2024
- Matokeo ya Safari Champions vs Yanga Sc Leo 29 June 2024
- Picha Za Parade ya Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24
- Yanga SC Kusherehekea Ubingwa wa Ligi kwa Parade Kubwa Mei 25
- Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2023/24: Ushindi wa Mara ya 30 Kihistoria
Weka Komenti