Taifa Stars Yashuka Nafasi Nne Katika Orodha Mpya ya Viwango vya FIFA
Dar es Salaam, Septemba 18, 2025 – Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeshuka kwa nafasi nne kwenye viwango vipya vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA Rankings) vilivyotangazwa leo. Stars sasa inashika nafasi ya 107 duniani na 22 barani Afrika, ikitoka nafasi ya 103 katika viwango vya mwezi Julai.
Kuporomoka huko kunahusishwa na matokeo yasiyoridhisha kwenye michezo miwili ya kufuzu Kombe la Dunia 2026. Taifa Stars ilitoka sare ya bao 1–1 dhidi ya Congo ugenini kabla ya kupoteza kwa bao 1–0 nyumbani dhidi ya Niger, matokeo yaliyopunguza pointi zake kwenye hesabu za ubora wa FIFA.
Nafasi za Majirani wa Tanzania
Wakati Stars ikiporomoka, Uganda (The Cranes) imeonyesha maendeleo makubwa baada ya kupanda kutoka nafasi ya 88 hadi 82 duniani, ikiwa ya 15 barani Afrika. Mnyo na Somalia walilazimika kuikubali Cranes katika michezo ya kufuzu Kombe la Dunia, hali iliyochangia ongezeko la pointi.
Kenya (Harambee Stars) kwa upande wake imeshuka kwa nafasi mbili, sasa ikiwa 111 duniani na 26 barani Afrika, licha ya kupata ushindi mmoja na kupoteza mmoja katika mechi zake mbili za kufuzu.
Mabadiliko ya Juu Duniani
Kwa upande wa 10 bora duniani, kumekuwa na mabadiliko muhimu. Uhispania imepanda hadi kileleni, ikimporomosha bingwa wa dunia Argentina hadi nafasi ya tatu, huku Ufaransa ikichukua nafasi ya pili. Orodha ya juu inaendelea na England katika nafasi ya nne, Ureno ya tano, ikifuatiwa na Brazil (6), Uholanzi (7), Ubelgiji (8), Croatia (9) na Italia (10).
Kinara Barani Afrika
Barani Afrika, Morocco inaendelea kushika uongozi ikiwa nafasi ya 11 duniani. Senegal inafuata ikiwa ya 18 kidunia, kisha Misri (35), Algeria (38) na Ivory Coast (44). Timu hizi zimeendelea kuimarisha nafasi zao kupitia matokeo mazuri kwenye mashindano ya bara na kufuzu Kombe la Dunia.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Benfica Yampa Mourinho Kibarua cha Kuiongoza kwa Miaka Miwili
- Yanga Yaanza Msimu wa Ligi ya Mabingwa Kwa Ushindi wa 3-0
- TRA Yaingia Rasmi Kwenye Michezo Baada ya Kuinunua Tabora United
- Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025
- Ratiba ya Mechi za CAF Leo 19 September 2025
- Gamondi Atamba na Singida BS Baada ya Kutwaa Ubingwa wa Haraka
- Ratiba ya Mechi za Leo 18 September 2025
- Simba SC Yaondoka na Kikosi cha Wachezaji 23 kuelekea Botswana Leo 17/09/2025
Leave a Reply