Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi
Mwisho wa Maombi Julai 21, 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu ā ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia baru ayenye Kumb. Na. FA.97/228/01/09 ya tarehe 25.06.2024. Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:-
- Mtendaji Wa Kijiji Daraja La Iii (Nafasi (09)
- Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La Ii (Nafasi 02)
- Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja La Ii (Nafasi 03)
- Dereva Daraja La Ii (Nafasi 4)
Sifa za Mwaombaji Nafasi za Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III
Kuajiriwa mwenye Elimu ya kidato cha IV, au VI aliyehitimu mafunzo ya Astashahada / cheti NTA LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo: ā Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa katika Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali
Sifa za Mwaombaji Nafasi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La II
Awe amehitimu kidato cha nne na mwenye stashahada (Diploma) ya uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile;Word, Excel, Power
Point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
Sifa za Mwaombaji Nafasi zaĀ Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja La II
Awe amehitimu Eimu ya kidato na nne [IV] au kidato cha sita [VI] na awe na Stashahada [NTA level 6] katika fani ya masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali, mwenye ujuzi wa kompyuta.
Sifa za Mwaombaji Nafasi zaĀ Dereva Daraja La II
Awe amehitimu na mwenye cheti cha kidato cha Nne ( Form IV ). Awe na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka bila kusababisha ajali.Na awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic
Driving Course) yanayotolewa na chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali.
Vitui Vya Kuingatia Wakati wa Kutuma Maombi Ya Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa aajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji aambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anawani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti ya kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Testmonialsā āProvisional Resultsā. Statement of Resultsā, hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) Ā HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.CCA.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Jinsi Ya Kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa āRecruitment Portalā)
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti