Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025 Saa Ngapi?

Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025 Saa Ngapi?

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo itarudi tena dimbani kuendelea na safari yake ya kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya mtoano ya AFCON 2025, itakapokutana uso kwa uso na Tunisia katika mchezo wa mwisho wa Kundi C. Mchezo huu umebeba uzito mkubwa kwa Taifa Stars, ambao kwa sasa wapo kwenye hesabu ngumu baada ya matokeo ya michezo miwili ya awali.

Kwa mashabiki wanaojiuliza “Tanzania vs Tunisia leo 30/12/2025 saa ngapi?” jibu ni kwamba mechi hiyo itapigwa leo kuanzia saa 1:00 usiku, huku ikirushwa mubashara kupitia Azam Sports 1 HD.

Tanzania vs Tunisia Leo Saa Ngapi na Wapi?

  • Mechi: Tanzania vs Tunisia
  • Mashindano: AFCON 2025
  • Kundi: C
  • Muda wa Kucheza: Saa 1:00 usiku
  • Urushaji: Azam Sports 1 HD

Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025 Saa Ngapi?

Nafasi ya Taifa Stars Kwenye Kundi C

Taifa Stars inaingia kwenye mechi hii ikiwa kwenye presha kubwa baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ kwenye mchezo uliopita. Sare hiyo imeifanya Tanzania ibaki na matumaini finyu ya kufuzu, kwa kuwa sasa italazimika kushinda dhidi ya Tunisia, huku ikiiombea Nigeria, ambayo tayari imeshafuzu, iifunge Uganda kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo.

Kwa upande wa Kundi C:

Nigeria tayari imefuzu hatua ya 16 bora baada ya kushinda mechi zake zote mbili, ikiifunga Tanzania mabao 2-1 na baadaye kuichapa Tunisia 3-2.

Taifa Stars chini ya kocha Miguel Gamondi, imeshindwa kushinda mechi yoyote hadi sasa, ikipata sare moja na kupoteza moja.

Tunisia nayo ipo kwenye presha, jambo linaloifanya mechi ya leo kuwa ya ushindani mkubwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Kundi C La Tanzania AFCON 2025
  2. Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Uganda Leo 27/12/2025
  3. Matokeo ya Uganda Vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025
  4. Uganda vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025 Saa Ngapi?
  5. Ratiba ya Mechi za AFCON Leo 27/12/2025
  6. Msimamo wa Makundi AFCON 2025
  7. Bao la Dakika za Mwisho la Patson Daka Lainusuru Zambia Dhidi ya Mali, Mechi Ikiisha 1-1
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo