Tarehe ya Kuripoti Makambini JKT Mujibu wa Sheria 2025

Tarehe ya Kuripoti Makambini JKT Mujibu wa Sheria 2025

Leo, tarehe 27 Mei 2025, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka huu ambao wanapaswa kuripoti katika makambi mbalimbali kwa ajili ya mafunzo ya lazima ya JKT kwa mujibu wa sheria. Maelfu ya wahitimu hao wamepangiwa makambi yaliyopo katika mikoa tofauti ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa kuwajengea vijana uzalendo, ujuzi wa maisha, na maandalizi ya kulihudumia Taifa.

Tarehe ya Kuripoti Makambini JKT Mujibu wa Sheria 2025

Tarehe ya Kuripoti Makambini Kwa Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Jeshi la Kujenga Taifa kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Juma Mrai, vijana wote waliomaliza kidato cha sita mwaka 2025 wanapaswa kuripoti katika makambi yao kati ya tarehe 28 Mei hadi 8 Juni 2025. Hii ni ratiba rasmi ya kuripoti na ni muhimu kwa wahusika wote kuzingatia tarehe hizi ili kuepuka usumbufu au adhabu zozote zinazoweza kutolewa kwa kuchelewa.

Makambi ya JKT Waliyopangiwa Wahitimu

Jeshi la Kujenga Taifa limegawa wahitimu katika makambi mbalimbali nchini kulingana na uwezo na miundombinu ya kila kambi. Makambi hayo ni kama ifuatavyo:

  1. Mkoa wa Mara: Rwamkoma
  2. Mkoa wa Tabora: Msange
  3. Mkoa wa Pwani: Ruvu (Mlandizi) na Kibiti
  4. Mkoa wa Dodoma: Mpwapwa na Makutopora
  5. Mkoa wa Iringa: Mafinga
  6. Mkoa wa Ruvuma: Mlale
  7. Mkoa wa Tanga: Mpambo na Maramba
  8. Mkoa wa Arusha: Makuyuni na Orjolo
  9. Mkoa wa Kigoma: Bulombora, Kanembwa na Mtabila
  10. Mkoa wa Songwe: Itaka
  11. Mkoa wa Rukwa: Luwa na Milundikwa
  12. Mkoa wa Lindi: Nachingwea

Kwa vijana wenye ulemavu wa wazi (physical disabilities), wanatakiwa kuripoti katika Kambi ya Ruvu mkoani Pwani, kwa kuwa imeandaliwa kwa miundombinu rafiki kwa watu wa jamii hiyo.

Mavazi na Vifaa Muhimu vya Kuambatana Navyo

Vijana wote wanatakiwa kujiandaa kikamilifu kwa kuzingatia mahitaji ya mavazi na vifaa muhimu kama yalivyoelekezwa na Jeshi. Vitu vya msingi ni pamoja na:

  • Bukta ya buluu iliyokoza, yenye mpira kiunoni, mfuko mmoja nyuma, isiyo na zipu, urefu wake uishie magotini.
  • Fulana ya kijani
  • Raba za michezo zenye rangi ya kijani na bluu
  • Shuka mbili za buluu bahari
  • Soksi ndefu nyeusi
  • Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye hali ya hewa ya baridi
  • Traki suti ya kijani au bluu
  • Vijana pia wanapaswa kubeba nyaraka muhimu kama:
  • Cheti cha kuzaliwa
  • Vyeti vya kuhitimu kidato cha nne
  • Nauli ya kwenda kambini na kurudi nyumbani
  • Nyaraka za msingi za udahili kwa elimu ya juu

Namna ya Kuangalia Kambi Uliyopangiwa

Kwa wanafunzi wanaotaka kujua kambi walikopangiwa, wanashauriwa kutembelea tovuti rasmi ya JKT kupitia kiungo: www.jkt.mil.tz. Katika tovuti hiyo, mwanafunzi ataingiza jina la shule pamoja na namba ya shule alikosomea kidato cha sita, kisha ataweza kuona taarifa kamili ya uteuzi wake, kambi aliyopangiwa pamoja na mkoa na wilaya inayohusika.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vitu vya Kwenda Navyo JKT Mujubu Wa Sheria 2025
  2. Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 Mujibu wa Sheria
  3. Ni Lini TAMISEMI Itatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026?
  4. Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026
  5. Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)
  6. Waliochaguliwa Kidato cha Tano Mkoa wa Dodoma 2025/2026
  7. Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano Dar es Salaam 2025/2026
  8. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo