Tarehe ya Kutangazwa kwa Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 na NECTA
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita kwa mwaka 2025 leo tarehe 07 Julai, katika hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar. Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed, alieleza kuwa jumla ya watahiniwa wa shule 125,779 sawa na asilimia 99.95% ya waliopata matokeo, wamefaulu mtihani huo.
Akiongeza kuwa watahiniwa 68 sawa na asilimia 0.05% hawakufaulu, Dkt. Said alifafanua kuwa ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 0.03% ikilinganishwa na mwaka 2024 ambapo ufaulu ulikuwa 99.92%.
Hata hivyo, katika hatua ya kuhakikisha uadilifu wa mitihani unaendelea kulindwa, NECTA imetangaza kufuta matokeo ya watahiniwa 71 waliobainika kufanya udanganyifu. Kati yao, 70 ni wa Mtihani wa Kidato cha Sita (ikiwa ni 64 wa shule na 6 wa kujitegemea), huku mmoja akiwa ni wa Mtihani wa Ualimu Daraja A (GATCE).
Dkt. Said amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5(2)(i) na (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani Sura ya 107, kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani za mwaka 2016.
Wazazi, wanafunzi, na wadau wa elimu wanakumbushwa kuzingatia umuhimu wa uadilifu katika mitihani, kwani matokeo ya udanganyifu yanakabiliwa na hatua kali za kisheria.
Lengo la Mtihani wa ACSEE (Kidato cha Sita)
Mtihani wa Kidato cha Sita, ambao kitaalamu unajulikana kama Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE), unalenga kutathmini kiwango cha maarifa cha wanafunzi pamoja na uwezo wao wa kuendelea na elimu ya juu. Lengo kuu la mtihani huu ni:
- Kupima uwezo wa mwanafunzi kujiunga na elimu ya juu kama shahada au diploma.
- Kuwezesha mwanafunzi kutumia ujuzi alioupata kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kisiasa, na kiteknolojia.
- Kuthibitisha umahiri wa mwanafunzi katika kutumia maarifa katika nyanja mbalimbali za maisha.
Kwa msingi huo, watahiniwa wa Kidato cha Sita wanatarajiwa kuonesha uelewa wa kina kupitia viwango mbalimbali vya maarifa ikiwa ni pamoja na: kufahamu, kutumia, kuchambua, kuunganisha mawazo, na kutoa tathmini sahihi ya hoja mbalimbali.
Tarehe Inayotarajiwa ya Kutangazwa kwa Matokeo ya Kidato cha Sita 2025
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dr. Said Mohammed ametangaza matokeo ya kidago cha sita leo July 07,2025 Visiwani Zanzibar ambapo kati Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 125,779 sawa na 99.95% ya Watahiniwa wenye matokeo.
Matokeo ya Kidato cha Sita: Mwenendo wa Matangazo ya NECTA kwa Miaka ya Nyuma
Kwa mujibu wa takwimu za miaka ya nyuma, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) mara nyingi hutangaza Matokeo ya Kidato cha Sita katika kipindi cha Julai, hasa kati ya tarehe 10 hadi 20. Hii ni kwa mujibu wa ratiba rasmi ya elimu pamoja na mwenendo wa miaka mitano iliyopita.
Tarehe za Kutangazwa Matokeo kwa Miaka ya Hivi Karibuni:
- Mwaka 2024: Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 yalitangazwa Jumamosi, Julai 13, 2024.
- Mwaka 2023: Matokeo yalitangazwa Julai 13, 2023.
- Mwaka 2022: Matokeo yalitangazwa Jumanne, Julai 5, 2022.
- Mwaka 2021: Matokeo yalitangazwa Jumamosi, Julai 10, 2021.
- Mwaka 2020: Matokeo yalitangazwa Ijumaa, Agosti 21, 2020 (tarehe hii ilibadilika kidogo kutokana na athari za janga la COVID-19, ikitoa uzoefu wa kipekee).
Kwa msingi huo, kuna ushahidi thabiti kuwa NECTA hufuata utaratibu wa kutangaza matokeo ya Kidato cha Sita katika wiki ya pili ya Julai kila mwaka.
Je, Ni Lini Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 Yatatarajiwa Kutangazwa Rasmi?
Hadi sasa, NECTA haijatoa tarehe rasmi ya kutangazwa kwa matokeo ya Kidato cha Sita 2025. Hata hivyo, kwa kuzingatia historia ya miaka iliyopita pamoja na muktadha wa ratiba ya kitaifa ya elimu kwa mwaka 2025/2026, kuna uwezekano mkubwa kuwa Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 yatatangazwa kati ya tarehe 10 hadi 20 Julai 2025.
Wahitimu na wadau wa elimu wanashauriwa kufuatilia kwa karibu tovuti rasmi ya NECTA pamoja na vyombo vya habari vya kuaminika kwa taarifa sahihi.
🔗 Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA kwa matangazo mapya ya matokeo.
Umuhimu wa Matokeo ya Kidato cha Sita kwa Mustakabali wa Elimu ya Juu
Matokeo haya hutumika kama kigezo kikuu cha uandikishaji katika vyuo vikuu, vyuo vya elimu ya ufundi, na taasisi nyingine za elimu ya juu. Wahitimu ambao hupata alama za juu hupata nafasi kubwa ya kuchaguliwa kujiunga na programu mbalimbali za kitaaluma. Mitihani hii hujulikana rasmi kama ACSEE – Advanced Certificate of Secondary Education Examination, ambayo huwapima wanafunzi katika:
- Maarifa ya jumla (General Studies)
- Mchepuo wa Sayansi (kama PCM, PCB, EGM)
- Mchepuo wa Sanaa na Biashara (kama HGK, HGE, ECA)
Lengo ni kupima uwezo wa mwanafunzi kuendelea na masomo ya juu pamoja na kutumia maarifa kutatua changamoto za kijamii, kiuchumi, na kiteknolojia.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
Je, matokeo ya Kidato cha Sita 2025 yametoka?
Hapana. NECTA bado haijatangaza rasmi tarehe ya matokeo.
Matokeo yanapatikana wapi?
Matokeo yatapatikana kwenye tovuti ya NECTA kupitia www.necta.go.tz
Ni lini NECTA huwa inatangaza matokeo kwa kawaida?
Kwa miaka mingi iliyopita, matokeo ya Kidato cha Sita hutangazwa kati ya Julai 10–20.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Lionel Messi anukia Ligi Kuu ya Uingereza EPL
- Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily ya Misri Baada ya Kuipa Yanga Mataji 3
- Simba SC Yapiga Hesabu Kumnasa Balla Moussa Conte Kutoka Sfaxien
- Simba SC Yamalizana na Ayoub Lakred Huku Hatma ya Camara Ikiwa Gizani
- Makombe ya Yanga 2024/2025
- Timu zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Dunia Vilabu 2025
- Chelsea Yamwaga Paundi Milioni 60 Kumsajili Mshambuliaji Joao Pedro
Leave a Reply