Mgunda Atajwa Kuchukua Mikoba ya Zahera Namungo
Baada ya kuuanza msimu kwa mwatokeo yasio rizisha, Namungo FC, inasemekana kuwa kwenye mazungumzo na kocha wa timu ya wanawake ya Simba Queens, Juma Mgunda, ili aweze kuchukua nafasi ya kocha wa sasa, Mwinyi Zahera. Hii inafuatia matokeo yasiyoridhisha katika mechi mbili za mwanzo za ligi kuuu msimu huu mpya wa 2024/2025.
Namungo FC imeanza msimu kwa kushindwa katika mechi dhidi ya Tabora United kwa mabao 2-1, na kisha kupoteza tena kwa Fountain Gate kwa mabao 2-0. Matokeo haya yameleta mabadiliko ya uongozi, ambapo Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Omar Kaya, alitangaza kujiuzulu baada ya kipigo cha pili. Hii imepelekea uongozi wa klabu hiyo kuanza mchakato wa kutafuta kocha mpya.
Juma Mgunda Apendekezwa Kuinoa Namungo FC
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Namungo FC, mmoja wa viongozi wakuu wa klabu hiyo alimpigia simu Juma Mgunda kumtaka aje kuiongoza timu hiyo. Inasemekana tayari mazungumzo na kocha Zahera yameshakamilika, na kilichobaki ni tangazo rasmi la kuondoka kwake.
Chanzo kimoja kilifichua kuwa Mgunda anaweza kuleta msaidizi wake Ngawina Ngawina, ambaye kwa sasa anafanya kazi na Coastal Union, iwapo atakubaliana na dili hilo. Sababu kubwa inayotajwa kwa Namungo kumhitaji Mgunda ni uzoefu wake wa muda mrefu kwenye soka, kuanzia kufundisha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, hadi kuinoa Simba SC kipindi cha mpito baada ya kuondoka kwa kocha Zoran Maki.
Katibu wa klabu ya Namungo, Ally Seleman, alipoulizwa kuhusu tetesi hizi, alikiri kuwa habari hizo zimezagaa, lakini alisisitiza kuwa hakuna lolote lililothibitishwa rasmi. Alisema kwamba ni suala la kusubiri na kuona kinachoweza kutokea katika siku chache zijazo.
“Hizo ni tetesi ambazo siwezi kusema ndio ama hapana, tusubiri muda utaongea nadhani kuanzia kesho (leo) Jumatatu ukweli utajulikana,” alisema Seleman.
Mgunda Pia Atajwa Azam FC
Mbali na Namungo FC, inasemekana Azam FC, klabu yenye mafanikio makubwa nchini, pia inamtazama Mgunda kama mbadala wa kocha wao wa sasa, Youssouf Dabo. Dabo anadaiwa kuwa kwenye hatihati ya kupoteza nafasi yake baada ya Azam FC kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 2-1.
Kwa muhtasari, hatima ya Juma Mgunda katika soka la Tanzania inatarajiwa kujulikana hivi karibuni. Namungo FC na Azam FC zote zinaonyesha nia ya kumpa majukumu mapya, jambo linalowafanya mashabiki wa soka kusubiri kwa hamu kuona uamuzi wa mwisho.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Manuel Ugarte Apewa Jezi Namba 25 ya Man United, Jezi ya Zamani ya Jadon Sancho
- Vigogo KenGold Waeka Dau Kubwa kwa Kila Ushindi
- JKU FC Mabingwa Wa Ngao ya Jamii Zanzibar 2024
- Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
- Chelsea Yamnasa Jadon Sancho kutoka Man Utd kwa Dili la Mkopo
- Azimio Bingwa Ndondo Cup 2024
Weka Komenti