Tarehe ya Kutangazwa Selection Za Kidato cha Tano 2025 | Tarehe ya Kutoka Selection 2025
Selection za Kidato cha Tano 2025, ambazo pia hujulikana kama uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na elimu ya sekondari ya juu, ni mchakato wa elimu unaosubiriwa kwa shauku kubwa kila mwaka, hususan na wahitimu wa kidato cha nne.Zoezi hili husimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, likiwa na lengo la kuhakikisha wanafunzi waliopata matokeo mazuri katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne (NECTA) wanapewa nafasi ya kujiendeleza kielimu kwa kupangiwa shule za sekondari za serikali au vyuo vya kati kwa mwaka wa masomo unaofuata.
Mwaka huu wa 2025, kama wewe ni mzazi, mlezi au mwanafunzi unaesubiri matokeo ya uchaguzi huu, basi makala hii itakupa mwongozo wa kina kuhusu matarajio ya tarehe rasmi ya kutangazwa kwa selection za kidato cha tano na vyuo vya kati, vigezo vinavyotumika kuchagua wanafunzi, na namna ya kuangalia majina ya waliochaguliwa mtandaoni.
Tarehe ya Kutangazwa Selection Za Kidato cha Tano 2025
Kwa kuzingatia utaratibu wa miaka ya nyuma uliowekwa na TAMISEMI, majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 yanatarajiwa kutangazwa kati ya tarehe 25 Mei hadi 15 Juni 2025.
Hii ni baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa matokeo ya kidato cha nne kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Ni vyema wazazi, walezi na wanafunzi kufuatilia taarifa rasmi kupitia tovuti ya TAMISEMI ili kuhakikisha hawakosi tangazo hilo muhimu.
TAMISEMI inazingatia masharti maalum ya ufaulu ili kuwachagua wanafunzi watakaoendelea na elimu ya sekondari ya juu. Vigezo hivi vinafafanua nani anastahili kupewa nafasi ya kuendelea na masomo:
1. Ufaulu wa Masomo Yasiyopungua Matatu kwa Daraja la Credit
Mwanafunzi anatakiwa awe amefaulu angalau masomo matatu kwa alama ya A, B au C – hii haijumuishi masomo ya dini.
2. Jumla ya Alama Katika Masomo Saba Isizidi 25
Kigezo hiki inahakikisha mwanafunzi ana kiwango bora cha ufaulu katika masomo yote aliyofanya kwenye mtihani wa kidato cha nne.
3. Ufaulu Katika Masomo ya Tahasusi (Combination)
Ili kuchaguliwa kwa tahasusi fulani, mwanafunzi anatakiwa kuwa na alama za 3 hadi 10 kwenye masomo ya tahasusi. Aidha, alama ya F kwenye masomo hayo hairuhusiwi.
4. Umri Usiozidi Miaka 25
TAMISEMI huwapangia shule wanafunzi wenye umri wa chini ya miaka 25.
5. Ushindani na Nafasi Zilizopo Mashuleni
Mchakato wa uchaguzi huzingatia ushindani kulingana na nafasi zilizopo kwenye shule mbalimbali.
6. Wanafunzi wa Shule Binafsi au Nje ya Mfumo Rasmi
Kwa wanafunzi waliopata matokeo kutoka nje ya mfumo rasmi, uchaguzi wao hutegemea ulinganifu wa matokeo hayo kwa mujibu wa NECTA.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025
Mara baada ya kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa, unaweza kuyapata kwa njia rahisi kupitia mtandao wa TAMISEMI. Fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI kupitia kiungo: www.tamisemi.go.tz
- Bonyeza sehemu iliyoandikwa “Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025”
- Chagua mkoa, halmashauri, na shule ya sekondari uliyosoma
- Angalia jina lako kwenye orodha itakayooneshwa
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ni Lini TAMISEMI Itatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026?
- Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Jeshi la Polisi 2025
- Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2025/2026
- Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)
- Vitu vya Kwenda Navyo JKT Mujibu Wa Sheria 2025
- Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 Mujibu wa Sheria
- Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026
- Tarehe ya Kuripoti Makambini JKT Mujibu wa Sheria 2025
Leave a Reply