Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 | Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25: Pata habari zote kuhusu Tetesi Simba, Yanga, Azam na Vilabu Vingine ligi kuu ya NBC.

Dirisha la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25 limefunguliwa rasmi tarehe 15 Juni 2024, na klabu mbalimbali zimeanza harakati za kuimarisha vikosi vyao kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 2024. Mashabiki wa soka nchini wamekuwa na hamu kubwa ya kujua ni wachezaji gani wapya watasajiliwa na klabu zao pendwa, huku wakijiuliza pia ni akina nani wataondoka.

Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 zimezagaa mitandaoni kuhusu mipango ya usajili wa vigogo wa soka nchini, Simba SC, Young Africans SC, na Azam FC. Je, Simba watafanikiwa kumsajili mshambuliaji wao anayetamaniwa na wengi? Yanga watatimiza ahadi zao za usajili wa wachezaji wazuri aina ya Aziz Ki? Azam wataendelea kutawala kwa kusajili nyota wapya?

Makala haya yanakuletea habari za hivi punde kuhusu tetesi za usajili zinazotikisa Ligi Kuu Tanzania Bara. Tutatazama kwa undani mipango ya usajili wa Simba, Yanga, Azam, Singida Black Star, Coastal union na klabu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ya NBC. Je, ni usajili gani wa kushtukiza unaoweza kutokea? Ni wachezaji gani wanaotakiwa na vilabu vikubwa?

Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

  1. Kiungo mahiri wa Young Africans, Aziz Ki, ametia saini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
  2. Beki kisiki wa Coastal Union, Lameck Lawi, amekuwa kivutio kikubwa kwa Azam FC na Young Africans, huku klabu zote mbili zikipania kumsajili.
  3. Winga machachari wa Simba SC, Aubin Kramo, huenda akaelekea Zesco United ya Zambia kwa mkopo.
  4. Foday Trawally, kiungo mchezeshaji mwenye kipaji kutoka Gambia, yuko mbioni kujiunga na Simba SC kwa mkataba wa miaka mitatu.
  5. Simba SC inahusishwa na usajili wa beki wa kati wa Asec Mimosas, Anthony Tra Bi Tra.
  6. Young Africans inammezea mate kiungo mkabaji wa Singida Black Stars, Yusuph Kagoma, kama mbadala wa Zawadi Mauya anayetarajiwa kuondoka.
  7. Simba SC inataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Raja Casablanca, Abdelhay Forsy.
  8. Singida Black Stars imekamilisha usajili wa mlinda mlango Mohamed Camara kutoka Horoya AC ya Guinea na inakaribia kumsajili beki wa kushoto, Imoro Ibrahim.
  9. Young Africans SC iko kwenye hatua za mwisho za kumsajili beki wa kushoto wa Asec Mimosas, Frank Zouzou.
  10. Beki mahiri wa kati kutoka Mauritania, Lamin Ba, yuko kwenye rada za Simba SC.
  11. Henock Inonga amejiunga na klabu ya Far Rabat.
  12. Simba SC inafikiria kumsajili beki wa RS Berkane, Issofou Dayo.
  13. Simba SC inamnyatia kiungo mshambuliaji, Augustine Okejepha.
  14. Simba SC inamwinda mshambuliaji hatari, Derick Fordojou.
  15. Kiungo Mkenya, Rodgers Torach, anafuatiliwa na Simba SC.
  16. Simba SC inamfuatilia kwa karibu Mohamed Damaro Camara.
  17. Daniel Msengani ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na Simba SC.
  18. Singida Black Stars inamtaka mshambuliaji Victorien Adebayor.
  19. Young Africans inamtaka Beno Kakolanya kuchukua nafasi ya Metacha Mnata.
  20. Mshambuliaji Jean Baleke yuko kwenye rada za Young Africans.
  21. Luis Jose Miquissone anawaniwa na APR ya Rwanda na timu kutoka Angola.
  22. Kiungo wa Coastal Union, Greyson Gelard, anawaniwa na Young Africans.
  23. Young Africans inamtaka mshambuliaji Duvan Elenga.
  24. Simba SC inamnyatia Flory Yangao.
  25. Skudu Makudubela huenda akaondoka Young Africans.
  26. Simba SC inamtaka Chance Leroy.
  27. Ayoub Lakred anahitajika na Wydad AC.
  28. Simba SC inamtaka mshambuliaji Mzambia Rick Banda.
  29. Omar Nahji anaweza kuchukua nafasi ya Bencharki Simba SC.
  30. Vilabu vya Al Qadsia ya Kuwait na Pyramids FC ya Misri vinamtaka Fabrice Ngoma wa Simba SC.
  31. Golikipa Yona Amos anakaribia kujiunga na Young Africans.
  32. Joshua Mutale anatakiwa kujiunga na Simba SC.
  33. Kelvin Kapumbu anatakiwa na Simba SC.
  34. Gnagna Barry na Mousa Camara wa Horoya AC wanawindwa na Simba SC.
  35. Ousmane Drame wa Horoya AC anawindwa na Simba SC.
  36. Saido Kanoute na Putin wanaweza kuondoka Simba SC kama mambo hayatabadilika.
  37. Mabululu anawaniwa na Simba SC na timu kutoka nchi za Kiarabu.
  38. Lameck Lawi anawaniwa na Simba SC.
  39. Frolent Ibenge anaweza kujiunga na Simba SC.
  40. Chadrack Boka amejiunga na Young Africans.
  41. Basiala Agee anahitajika na Young Africans.
  42. Aziz Andambwile anawaniwa na Simba SC kuchukua nafasi ya Abdallah Hamis.
  43. Keneth Semakula anawaniwa na Simba SC na Azam FC.
  44. Jhonier Blanco anaweza kuwa mrithi wa Dube Azam FC.
  45. Elia Mpanzu anakaribia kujiunga na Simba SC.
  46. Simba SC inajaribu kuingilia kati dili la Yusuph Kagoma kwenda Young Africans.
  47. Skauti wa Simba na FC Twente, Mels Daadler, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja.
  48. Kocha wa makipa wa Simba SC, Daniel Cadena, anakaribia kuondoka.
  49. Simba SC inamtaka kocha mkuu wa Petro Athletico, Alexander Santos.
  50. Omar Jobe ameondoka Simba SC.
  51. Steven Mukwara anawaniwa na Simba SC.
  52. Juma Mgunda anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu mpya wa Simba SC.
  53. Augustine Okrah ameondoka Simba SC.
  54. Kenedy Juma anakaribia kujiunga na Coastal Union.
  55. Miguel Gamondi atasalia Young Africans kwa mwaka mmoja zaidi.
  56. Winga Serge Pokou kutoka Asec Mimosas anakaribia kujiunga na Simba SC.
  57. Kocha Steve Komphela anaweza kujiunga na Simba SC.
  58. Barbara Gonzalez anakaribia kuchukua nafasi ya mtendaji mkuu wa Simba SC.
  59. Injinia Hersi Said hatokuwa tena mtendaji mkuu wa Simba SC.
  60. Manu Bora anawaniwa na Young Africans.
  61. Valentin Nouma anawaniwa na Simba SC.
  62. Joshua Mutale anawaniwa na Simba SC.
  63. Mohamed Damaro Camara anawaniwa na Simba SC.
  64. Kuna uwezekano mkubwa wa Juma Mgunda kurudi Coastal Union kwa mkopo.
  65. Banza Kalumba anawaniwa na Coastal Union.
  66. Beki wa kushoto wa KMC, Rahim Shomari, anawaniwa na Simba SC.
  67. Arthur Bada kutoka Ivory Coast anawaniwa na Simba SC.
  68. Soul Davilla anahusishwa na Simba SC.
  69. Kuna uwezekano mkubwa wa Jean Baleke kurejea Simba SC.
  70. Kelvin Kapumbu yupo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo kujiunga na Simba SC.
  71. Djuma Shaban amejiunga na Coastal Union.
  72. Young Africans yatajwa katika mbio za kuwinda saini ya George Mpole
  73. Kipa wa Simba, Ayoub Lakred, atasalia na klabu hiyo hadi 2025.
  74. David Luhende na Abdallah Seseme wamesaini na Dodoma Jiji FC.
  75. Kipa Msudani, Mohammed Mustapha, amesaini mkataba wa kudumu na Azam FC.
  76. William Togul Mel, straika kutoka Ivory Coast, yupo kwenye mazungumzo na Simba SC.
  77. Arthur Bada yupo katika mazungumzo na klabu ya Simba SC.
  78. Young Africans itamsajili Aboubakar Komen ikishindwa kumpata Yona Amos.
  79. Aubin Kramo ataendelea kuichezea Simba SC.
  80. Simba Sc yawinda saini ya Tandi Mwape
  81. Charles Ahoua amethibitishwa kusajiliwa na Simba SC.
  82. Kiungo wa Mashujaa FC, Omary Omary, anawaniwa na Simba SC.
  83. Young Africans na Singida Big Stars zipo kuchuana katika kuwania saini ya Yacoub Sogne

Soma Habari Kamili Kupitia Machapisho ha chini

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo