Timu Zilizofuzu Nusu Fainali COSAFA Cup 2025
Michuano ya COSAFA Cup 2025 hatimaye imefikia katika hatua ya kukatana shoka baada ya timu za mataifa mbalimbali kukamilisha mapambano katika hatua ya makundi, ambapo vinara wa makundi manne ndio waliopata tiketi ya kusonga mbele hadi hatua ya nusu fainali. Mashindano haya yaliyoandaliwa nchini Afrika Kusini yamekuwa na ushindani mkubwa huku matokeo ya kushtua na burudani ya kuvutia ikishuhudiwa katika kila mechi. Kwa mujibu wa matokeo ya makundi, timu nne zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuonyesha uwezo wa hali ya juu kwenye hatua ya awali.
Hizi ndizo timu zilizofanikiwa kuingia kwenye orodha ya wababe wa COSAFA Cup 2025:
- Madagascar
- Afrika Kusini
- Angola
- Comoros
Katika hatua ya nusu fainali, Madagascar watakipiga dhidi ya Angola katika mchezo wa fainali ya kwanza ya michuani hii unaotarajiwa kuamua nani atasonga mbele hadi fainali ya COSAFA Cup 2025.
Wakati huo huo, Afrika Kusini (Bafana Bafana B) watachuana na Comoros, mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa wenye mvuto zaidi kati ya wenyeji wa mashindano na timu inayopanda kwa kasi katika ukanda huu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Taifa Stars Yaaga COSAFA Cup Licha ya Kuifunga Eswatini 2-1
- Tijjani Reijnders Asaini Manchester City Miaka Mitano Akitokea AC Milan
- Serikali Yajieka Pembeni na Sakata la dabi, yawaachia TFF
- Chelsea Yathibitisha Kumsajili Beki Mamadou Sarr Kutoka Strasbourg
- Yanga Kususia Fainali CRDB FA Cup Kisa Madeni ya Msimu Uliopita
- Yanga Yaibua Mambo Mapya Wakizungumzia Sakata la Dabi
- Herry Sasii Afungiwa Soka Miezi 6 Kisa Mechi ya Simba na Singida
Leave a Reply