TRA United vs Simba SC Leo 09/04/2026 Saa Ngapi?

TRA United vs Simba SC Leo 09/04/2026 Saa Ngapi?

Wekundu wa Msimbazi leo watakuwa ugenini kuzisaka pointi tatu muhimu katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, ambapo Simba SC itashuka dimbani dhidi ya TRA United kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa jijini Arusha. Mchezo huu ni sehemu ya ratiba ya leo, Alhamisi Aprili 9, 2026, ukiwa ni kiporo kilichosogezwa mbele kutokana na mvua kubwa zilizonyesha wiki chache zilizopita.

TRA United vs Simba SC Leo Saa Ngapi?

  • TRA United vs Simba SC
  • Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
  • Muda Saa; 4:00 pm

TRA United vs Simba SC Leo 09/04/2026 Saa Ngapi?

Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na presha ya kurejea kwenye ushindi baada ya kuangusha pointi mbili mbele ya Azam, huku TRA United ikisaka kuvunja rekodi mbaya dhidi ya wapinzani hao. Tangu ipande Ligi Kuu, TRA haijawahi kuzuia Simba, jambo linaloifanya mechi hii kuwa na mvuto wa kipekee.

Katika takwimu za mikutano yao, Simba imekuwa na ubora mkubwa. Kabla ya mchezo huu, timu hizo zimekutana mara tano na Simba ikishinda zote, ikifunga mabao 15 huku TRA United ikiwa haijawahi kufunga hata bao moja. Ushindi mkubwa zaidi ulikuwa wa mabao 4-0 katika mchezo wao wa kwanza walipokutana wakati huo ikipewa jina la Tabora United.

Pamoja na rekodi hiyo, Simba imekuwa na changamoto katika mechi za ugenini msimu huu. Katika michezo mitano iliyopita ugenini, imeshinda miwili dhidi ya Tanzania Prisons kwa mabao 2-0 na Singida Black Stars kwa mabao 2-1, huku mingine mitatu ikiisha kwa sare dhidi ya Dodoma Jiji (1-1), Pamba Jiji (1-1) na Azam (0-0).

Habari njema kwa Simba ni kurejea kwa winga Elie Mpanzu, ambaye alikosa michezo miwili iliyopita kutokana na kuumwa. Mpanzu ana nafasi ya asilimia 50 kucheza mchezo huu, akiwa kinara wa kutengeneza mabao msimu huu kwa asisti tano, idadi inayolingana na Feisal Salum wa Azam FC.

Kocha wa Simba, Steve Barker, amesema wanatarajia mchezo mgumu dhidi ya TRA United lakini wamejipanga kurejea kwenye ushindi. “Utakuwa mchezo mgumu, tunakutana na TRA United inayocheza mpira mzuri, ina wachezaji wenye nguvu na kutokana na mchezo wa kwanza kuahirishwa na tulipowafunga nyumbani itaufanya mchezo huu kuwa na presha yake lakini tunataka kushinda turudi kwenye njia ya ushindi,” alisema Barker.

Kwa upande wa TRA United, timu hiyo chini ya kocha Ettiene Ndayiragije imekuwa na matokeo mazuri ya nyumbani, ikiwa imeshinda mechi tatu kati ya tano, sare moja na kupoteza moja. Hata hivyo, itawakosa Chamou Karaboue na Mzamiru Yassin kutokana na masharti ya mikataba yao ya mkopo.

Ndayiragije amesema wanaifahamu Simba kama timu kubwa yenye wachezaji wenye uzoefu, lakini wataingia uwanjani na mkakati wa kuzuia ubora wao na kutumia makosa yao kupata matokeo. “Simba ni moja kati ya timu kubwa hapa Tanzania, ina wachezaji wenye uzoefu mkubwa lazima uwe na hesabu nzuri, tutajaribu kuzuia yale ambayo yanawapa ubora lakini pia tutumie makosa yao kuweza kutengeeneza ushindi wetu,” alisema Ndayiragije.

Kabla ya mchezo huo, Bodi ya Ligi Tanzania ilitoa taarifa kuhusu tiketi, ikiwakumbusha mashabiki waliokata tiketi za mchezo uliokuwa umeahirishwa Machi 14 kuwa wataingia kwa kutumia tiketi hizo hizo bila kununua mpya, mradi wawe na kadi walizotumia awali. Wale ambao hawakununua tiketi kwenye mchezo wa kwanza wanatakiwa kununua tiketi mpya kwa mechi ya leo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  2. Matokeo ya Pamba Jiji vs Yanga Leo 08/04/2026
  3. Harry Maguire Asaini Mkataba Mpya Manchester United Hadi 2027
  4. AFCON 2027 Kufanyika Mwezi Juni na Julai
  5. Droo ya Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza: Man City Yapangwa na Southampton, Chelsea Uso kwa Uso Dhidi ya Leeds
  6. Timu Zilizofuzu Robo Fainali FA Cup Pemba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo