Viingilio Mechi ya Marudiano Simba Vs RS Berkane 25/05/2025
Viingilio vya mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF kati ya Simba SC dhidi ya RS Berkane, ambao utapigwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar, tarehe 25 Mei 2025, vimetangazwa rasmi huku mashabiki wakihimizwa kujiandaa mapema kushuhudia pambano hilo la kihistoria.
Mchezo huo wa fainali, unaotarajiwa kuanza saa 10:00 jioni (1600 HRS), ni sehemu ya michuano ya CAF Confederation Cup msimu wa 2024/2025 na unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi kutoka Tanzania na nje ya mipaka yake kutokana na uzito wa mchuano huo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka klabu ya Simba SC, tiketi za kuingia uwanjani zitapatikana kwa madaraja tofauti kama ifuatavyo:
Madaraja ya Tiketi na Bei Zake:
VIP A – Tsh 50,000
Kwa mashabiki wanaotaka huduma za kiwango cha hali ya juu na siti nzuri kabisa ya kutazama mchezo huu wa fainali, sehemu ya VIP A ndio0 mahali patakapo wapa mazingira bora zaidi na ya kifahari.
VIP B Urusi – Tsh 30,000
Hili ni chaguo la kati kwa mashabiki wanaotaka mchanganyiko wa starehe na unafuu wa bei, huku wakipata mandhari ya kuvutia ya uwanja.
Mzunguko Orbit – Tsh 10,000
Hiki ndicho kiwango cha chini cha kiingilio, kinachowapa nafasi mashabiki wengi zaidi kushiriki na kuisapoti timu yao ya Simba katika mchezo huu muhimu.
Mashabiki wanakumbushwa kununua tiketi mapema kupitia vituo rasmi vilivyotangazwa na klabu ili kuepuka usumbufu na ulanguzi wa tiketi. Kutokana na ukubwa wa mchezo, idadi ya mashabiki inatarajiwa kuwa kubwa, hivyo ni muhimu kupanga mapema kuhudhuria. Mchezo huu ni wa marudiano, na unatarajiwa kuamua bingwa wa Kombe la Shirikisho kwa msimu huu. Simba SC, wakiwa na historia ya kuvutia kwenye mashindano ya CAF, wanaingia uwanjani kwa matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi mbele ya mashabiki wao visiwani Zanzibar.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Muonekano wa Kombe Jipya La Klabu Bingwa CAF Champions League
- Dk. Mwinyi Ailipa Simba Ada ya Uwanja Fainali Kombe la Shirikisho!
- Kikosi cha RS Berkane Chatua Tanzania Kikiwa na Presha ya Simba Jumapili
- Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano Geita 2025/2026
- Kikosi Cha Simba VS RS Berkane Leo 17/05/2025 Fainali
- Bologna Yaichapa AC Milan na Kubeba Taji la Copa Italia 2025 Baada ya Ukame wa Miaka 51
- Refa Aliyekataa Bao la Aziz Ki Apewa Mechi ya Simba Nyumbani CAF
Leave a Reply