Vikosi Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024 | Kikosi cha Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons
Pazia la Ligi Kuu ya NBC Tanzania msimu wa 2024/2025 litafunguliwa rasmi tarehe 16 Agosti 2024 kwa pambano kali kati ya Pamba Jiji na Tanzania Prisons. Mchezo huu wa ufunguzi utapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, majira ya saa 10 jioni. Mashabiki wa soka nchini wanatarajia mechi hii kuwa na ushindani mkubwa kutokana na maandalizi na usajili wa nguvu uliofanywa na timu zote mbili.
Pamba Jiji: Historia na Matarajio
Pamba Jiji ni timu yenye historia ndefu katika soka la Tanzania, lakini msimu uliopita wa 2023/2024 walikuwa wakipambana katika Ligi Daraja la Kwanza (Championship). Walimaliza msimu huo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kupanda daraja, jambo linalowafanya kuwa na morali kubwa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu. Mashabiki wa Pamba Jiji wanatarajia kuanza ligi kwa ushindi, wakitegemea kuwa na kikosi imara kitakachoweza kupambana na miamba ya Ligi Kuu.
Tanzania Prisons: Changamoto na Malengo
Tanzania Prisons, ambao wamekuwa washiriki wa kudumu wa Ligi Kuu, wapo tayari kwa msimu mpya na wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Pamba Jiji. Kwa kuwa na uzoefu wa kucheza Ligi Kuu kwa miaka kadhaa, Tanzania Prisons wanaingia katika mchezo huu wakiwa na nia thabiti ya kuhakikisha wanapata pointi zote tatu na kuanza msimu mpya kwa mafanikio.
Vikosi Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024
Vikosi vya mechi ya pamba jiji vs tanzania prisons vinatarajiwa kutangazwa lisaa kabla ya mchezo kuanza na makocha wa pande zote mbili. Hapa tutakuletea kikosi cha pamba jiji vs tanzania prisons pamoja na kikosi cha tanzania prisons vs pamba jiji mara tu baada ya kutangazwa rasmi. Makocha wa timu zote mbili wamekuwa wakifanya mazoezi ya mwisho kwa kujipanga kikamilifu kuhakikisha wanateua wachezaji bora zaidi kwa ajili ya pambano hili. Ni wazi kwamba mbinu na mikakati itakayowekwa na makocha itakuwa na nafasi kubwa katika kuamua matokeo ya mchezo huu.
Viingilio na Namna ya Kukata Tiketi
Mashabiki watakaohudhuria mchezo huu wana fursa ya kuchagua viingilio vinavyowafaa. Viingilio ni kama ifuatavyo:
- VIP: TZS 10,000
- Jukwaani: TZS 5,000
- Mzunguko: TZS 2,000
Kwa wale ambao hawajakamilisha ununuzi wa tiketi mapema, tiketi zinapatikana katika maeneo yafuatayo:
- Ofisi kuu za Halmashauri ya Jiji Mwanza
- Ofisi za TTCL-Mwanza
- Uwanja wa CCM Kirumba
- Gari ya Matango
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti