Vituo Vya Kununua Tiketi za Mechi ya Yanga vs Simba 08/03/2025

Vituo Vya Kununua Tiketi za Mechi ya Yanga vs Simba 08/03/2025

Kama wewe ni shabiki wa dhati wa soka la Tanzania, basi huwezi kukosa mtanange wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba. Mechi hii inayozingatiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi katika soka la Afrika Mashariki na Kati, inatarajiwa kupigwa tarehe 08 Machi 2025 saa 1:15 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kwa mashabiki wanaotaka kuhudhuria mchezo huu utakao kua na ushindani na radha ya aina yake, ni muhimu kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho.

Hapa tumekuandalia orodha ya vituo rasmi vya kuuza tiketi kwa ajili ya mchezo huu wa kukata na shoka:

Vituo Rasmi vya Kununua Tiketi

  • Young Africans – Jangwani
  • Vunja Bei – Dar Es Salaam Shops
  • T-Money Ltd – Kigamboni
  • Gitano Samweli – Mbagala Zakiem
  • Khalfan Mohamed – Ilala
  • Lampard Electronics
  • Gwambina Lounge – Gwambina
  • Karoshy Pamba – Dar Live (Zakhiem)
  • Antonio Service – Sinza, Kivukoni
  • Tumpe Kamwela – Kigamboni
  • Sovereign – Kinondoni Makaburini
  • View Blue Skyline – Mikocheni
  • Mkaluka Traders – Machinga Complex
  • New Tech General Traders – Ubungo
  • Sabana Business – Mbagala Maji Matitu
  • Juma Burrah – Kivukoni
  • Juma Burrah – Msimbazi
  • Alphan Hinga – Ubungo
  • Mtemba Service Co – Temeke
  • Jackson Kimambo – Ubungo
  • Shirima Shop – Leaders

Vituo Vya Kununua Tiketi za Mechi ya Yanga vs Simba 08/03/2025

Muda wa Mechi na Umuhimu wa Kufika Mapema

Kwa kuwa hii ni mechi kubwa inayopendwa na wengi, inashauriwa kununua tiketi mapema na kufika uwanjani kwa wakati ili kuepuka msongamano. Tiketi zinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwa hapo juu, hivyo hakikisha unanunua kutoka kwa wauzaji rasmi ili kuepuka tiketi bandia. Mechi hii inatajwa kuwa na ushindani mkubwa, huku Yanga ikitaka kudumisha rekodi nzuri dhidi ya Simba katika msimu huu wa 2024/2025. Kwa upande mwingine, Simba SC italenga kulipiza kisasi baada ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa bao 1-0.

Mashabiki wa soka wanashauriwa kufuata taratibu zote za usalama na kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hili la kihistoria. Nunua tiketi yako mapema na ujiandae kwa burudani ya aina yake kwenye dimba la Benjamin Mkapa!

  • Tarehe ya Mechi: 08 Machi 2025
  • Saa: 1:15 Usiku
  • Uwanja: Benjamin Mkapa Stadium

Hakikisha haupitwi na tukio hili la kusisimua kwa kununua tiketi mapema!

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Bei ya Viingilio Mechi ya Yanga Vs Simba Leo 08/03/2025
  2. Yanga VS Simba Leo 08/03/2025 Saa Ngapi?
  3. Tabora United Kuwakabili JKT Tanzania CCM Kirumba Machi 7, 2025
  4. Bodi ya Ligi TPLB Yatangaza Tarehe Mpya ya Mechi ya Simba na Dodoma
  5. Timu Zilizofuzu 16 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup 2024/2025
  6. Mechi za Yanga Zilizobaki Ligi Kuu NBC 2024/2025
  7. Ratiba ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup Leo 03/03/2025
  8. Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025
  9. Mbeya City Yaing’oa Azam CRDB Bank Federation Cup kwa Mikwaju ya Penati
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo