Viwango Vya FIFA Duniani 2025 (FIFA Rankings)

Viwango Vya FIFA Duniani 2025 (FIFA Rankings)

TIMU ya taifa ya Hispania imeipokonya Argentina nafasi ya kwanza katika viwango vipya vya FIFA kwa timu za wanaume vilivyotolewa Alhamisi, 18 Septemba 2025. Hii ni mara ya kwanza kwa “La Roja” kuongoza dunia tangu Juni 2014. Ushindi wa Hispania katika mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Uturuki na Bulgaria umeihakikishia pointi 1,875.37 na kuipandisha juu ya wapinzani wao wakuu.

Argentina, bingwa wa Kombe la Dunia 2022, imeporomoka hadi nafasi ya tatu baada ya kupoteza dhidi ya Ecuador na kushinda mchezo mmoja pekee wa mwezi huu. Ufaransa imenufaika na hali hiyo kwa kupanda hadi nafasi ya pili kwa pointi 1,870.92, ikifuatiwa na England (nafasi ya 4) na Ureno (nafasi ya 5), ambayo imewapiku Brazil baada ya kupata matokeo mazuri kwenye michezo yake

Viwango Vya FIFA Duniani 2025 (FIFA Rankings)

Orodha ya Viwango Vya FIFA Duniani 2025 (FIFA Rankings)

Nafasi (RK) Timu Alama Jumla Alama za Awali Mabadiliko
1 Hispania (ESP) 1875.37 1867.09 +8.28
2 Ufaransa (FRA) 1870.92 1862.03 +8.89
3 Argentina (ARG) 1870.32 1885.36 -15.04
4 Uingereza (ENG) 1820.44 1813.32 +7.12
5 Ureno (POR) 1779.55 1770.53 +9.02
6 Brazil (BRA) 1761.60 1777.69 -16.09
7 Uholanzi (NED) 1754.17 1758.18 -4.01
8 Ubelgiji (BEL) 1739.54 1736.38 +3.16
9 Croatia (CRO) 1714.20 1707.51 +6.69
10 Italia (ITA) 1710.06 1702.58 +7.48
11 Morocco (MAR) 1706.27 1698.72 +7.55
12 Ujerumani (GER) 1704.27 1716.98 -12.71
13 Colombia (COL) 1692.10 1679.46 +12.64
14 Mexico (MEX) 1688.38 1689.73 -1.35
15 Uruguay (URU) 1673.65 1670.76 +2.89
16 Marekani (USA) 1670.04 1671.04 -1.00
17 Uswisi (SUI) 1648.30 1635.08 +13.22
18 Senegal (SEN) 1645.23 1635.10 +10.13
19 Japan (JPN) 1640.47 1641.23 -0.76
20 Denmark (DEN) 1627.64 1621.24 +6.40
21 Iran (IRN) 1622.61 1624.30 -1.69
22 Austria (AUT) 1601.86 1591.24 +10.62
23 Korea Kusini (KOR) 1593.19 1587.08 +6.11
24 Ecuador (ECU) 1588.04 1570.68 +17.36
25 Australia (AUS) 1583.49 1578.57 +4.92
26 Canada (CAN) 1558.04 1548.94 +9.10
27 Uturuki (TUR) 1555.72 1553.19 +2.53
28 Ukraine (UKR) 1543.06 1557.21 -14.15
29 Panama (PAN) 1529.71 1545.08 -15.37
30 Wales (WAL) 1529.09 1528.93 +0.16

Nafasi za Timu za Afrika na Asia

Morocco (Maroko) imeendelea kuwa kinara wa Afrika kwa kushika nafasi ya 11 duniani ikiwa na pointi 1,706.27. Senegal imepanda hadi nafasi ya 18 baada ya kushinda michezo mingi ya kimataifa.

Kwa bara la Asia, Japan inaongoza kwa kushika nafasi ya 19, ikifuatiwa na Iran (21) na Korea Kusini (23). Australia pia imeendelea kuimarika kwa kushika nafasi ya 25, huku Kanada (26) ikipanda kwa pointi 9.1 baada ya matokeo mazuri.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Benfica Yampa Mourinho Kibarua cha Kuiongoza kwa Miaka Miwili
  2. Yanga Yaanza Msimu wa Ligi ya Mabingwa Kwa Ushindi wa 3-0
  3. TRA Yaingia Rasmi Kwenye Michezo Baada ya Kuinunua Tabora United
  4. Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025
  5. Ratiba ya Mechi za CAF Leo 19 September 2025
  6. Gamondi Atamba na Singida BS Baada ya Kutwaa Ubingwa wa Haraka
  7. Ratiba ya Mechi za Leo 18 September 2025
  8. Simba SC Yaondoka na Kikosi cha Wachezaji 23 kuelekea Botswana Leo 17/09/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo