Wachezaji Wapya wa Yanga 2025/2026

Wachezaji Wapya wa Yanga 2025/2026 | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2025/2026

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, wameanza rasmi kutambulisha wachezaji wapya watakaokiongezea nguvu kikosi chao kwa msimu wa 2025/2026, ikiwa ni juhudi za kuhakikisha wanarudia mafanikio makubwa waliyoandika katika msimu wa 2024/2025, ambapo walitwaa mataji makubwa ya ndani na kuonyesha ushindani mkubwa kimataifa.

Katika hatua ya mwanzo ya dirisha la usajili, Yanga SC wamefanikiwa kumchukua rasmi kiungo mahiri wa kimataifa kutoka Guinea, Balla Moussa Conte, ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili. Conte ametambulishwa rasmi Ijumaa, huku akizua gumzo kubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa kuwa alikuwa akiwindwa vikali na watani wao wa jadi, Simba SC.

Mapambano ya Conte: Simba na Yanga Kwenye Vita ya Usajili

Kwa mujibu wa mchambuzi wa usajili Hans Raphael, Yanga SC ndiyo klabu ya kwanza nchini kuonesha nia ya kumsajili kiungo huyo kutoka klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia. Hata hivyo, baada ya taarifa hizo kuvuma, Simba SC waliingia katika kinyang’anyiro hicho kwa kasi kubwa kwa kuongea moja kwa moja na mawakala wa mchezaji kwa njia ya simu, wakiongozwa na kocha wao mkuu Fadlu Davis, aliyemtaja Conte kama chaguo lake namba moja sokoni msimu huu.

Ingawa Simba waliwasilisha ofa kubwa kwa CS Sfaxien, kulikuwa na tofauti kubwa ya masharti ya malipo. Simba walitaka kulipa kwa awamu mbili, jambo ambalo halikukubalika kwa klabu ya CS Sfaxien.

Yanga SC walikuja na ofa mpya iliyojumuisha malipo ya awamu moja, pamoja na ahadi ya kumpatia mchezaji huyo gari, nyumba, na mshahara mnono kitu kilichowavutia pande zote na kupelekea dili hilo kukamilika rasmi.

Wachezaji Wapya wa Yanga 2025/2026

Hans alifafanua:

“Baada ya vita kubwa kati ya Simba na Yanga, usiku wa jana Rais wa Yanga alituma ofa kubwa zaidi kwenda kwa Conte na CS Sfaxien. Ofa hiyo imekubalika na pande hizo mbili… Conte ameahidiwa na Yanga kupewa gari, nyumba ya kuishi na mshahara mnono.”

Yanga SC Yamgeukia Nahodha wa Simba – Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’

Mbali na kumtambulisha Conte, Yanga SC sasa wameelekeza macho yao kwa beki wa kushoto na nahodha wa Simba SC, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’. Inaripotiwa kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili tayari yameanza rasmi, na yanaendelea kwa mafanikio.

Kwa sasa, Zimbwe ni mchezaji huru, hivyo anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote. Habari kutoka kwa Hans Raphael zinaeleza kuwa kama makubaliano yatapatikana, mmoja wa viongozi wa Yanga atasafiri kwenda Misri, ambako Zimbwe yuko na kikosi cha timu ya taifa kilichoko kambini kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya CHAN, ili kumsainisha mkataba rasmi.

Hans alisema: “Niko hapa kuthibitisha dili la Zimbwe na Yanga bado halijakamilika, ila mazungumzo yanaendelea na yako katika hatua nzuri… Mwakala wake, Carlos ‘Mastermind’, ndiye anasimamia michakato yote ya kimkataba.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. CV ya Moussa Balla Conte Mchezaji Mpya wa Yanga Sc 2025/2026
  2. Tetesi za Usajili Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026
  3. Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
  4. Rasmi: Namungo FC Yathibitisha Kuachana na Mshambuliaji Meddie Kagere
  5. Kikosi cha Taifa Stars Kinaendelea Kujifua Nchini Misri kwa Ajili ya CHAN 2025
  6. Kocha wa Yanga Miloud Hamdi Ashinda Tuzo ya Kocha Bora wa NBC June 2024
  7. Simba Yathibitisha Kumtoa Omary Omary kwa Mkopo kwenda Mashujaa FC
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo