Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 – Pakua PDF Hapa!

Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 – Pakua PDF Hapa!

Leo tarehe 27 ya mwezi wa tano, mwaka 2025, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka huu, ambao wameteuliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria. Maelfu ya wahitimu hawa wa kidato cha sita wamepangiwa kuripoti katika makambi mbalimbali ya JKT yaliyosambaa katika mikoa tofauti ya Tanzania kwa ajili ya kushiriki katika mafunzo hayo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 - Pakua PDF Hapa!

Tarehe Rasmi za Kuripoti Kambini

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Mei 27, 2025 na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Kanali Juma Mrai kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele, vijana waliochaguliwa wanatakiwa kufika katika makambi yao kati ya tarehe 28 Mei hadi 8 Juni, 2025.

Orodha ya Makambi ya JKT na Mikoa Yake

Vijana walioteuliwa wamegawanywa katika makambi tofauti yaliyoko kwenye mikoa mbalimbali kama ifuatavyo:

  1. Mkoa wa Mara: Kambi ya Rwamkoma
  2. Mkoa wa Tabora: Kambi ya Msange
  3. Mkoa wa Pwani: Kambi ya Ruvu na Kibiti
  4. Mkoa wa Dodoma: Kambi ya Mpwapwa na Makutopora
  5. Mkoa wa Iringa: Kambi ya Mafinga
  6. Mkoa wa Ruvuma: Kambi ya Mlale
  7. Mkoa wa Tanga: Kambi ya Mpambo na Maramba
  8. Mkoa wa Arusha: Kambi ya Makuyuni na Orjolo
  9. Mkoa wa Kigoma: Kambi ya Bulombora, Kanembwa na Mtabila
  10. Mkoa wa Songwe: Kambi ya Itaka
  11. Mkoa wa Rukwa: Kambi ya Luwa na Milundikwa
  12. Mkoa wa Lindi: Kambi ya Nachingwea

Kwa vijana wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities), wanapaswa kuripoti Kambi ya Ruvu iliyopo Mlandizi, Mkoa wa Pwani ambayo ina miundombinu maalum ya kuhudumia watu wa aina hiyo.

Vifaa Muhimu vya Kubeba Wakati wa Kuripoti Kambini

Kwa mujibu wa Kanali Mrai, vijana wote wanaotakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT wanapaswa kufika wakiwa na vifaa maalum vilivyoainishwa kama ifuatavyo:

  1. Bukta ya rangi ya bluu iliyokoza yenye mpira kiunoni na mfuko mmoja nyuma (isiyo na zipu), urefu wa magotini.
  2. Fulana ya kijani.
  3. Raba za michezo zenye rangi ya kijani na bluu.
  4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya bluu bahari.
  5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa maeneo yenye hali ya baridi.
  7. Traki suti ya rangi ya kijani au bluu.

Nyaraka zote muhimu kama cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kidato cha nne na sita, pamoja na nauli ya kwenda kambini na kurudi.

Jinsi ya Kupata Orodha Kamili ya Majina ya Waliochaguliwa

Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa, makambi ya JKT waliyopangiwa, na vifaa vinavyotakiwa imewekwa kwenye tovuti rasmi ya Jeshi la Kujenga Taifa kupitia kiunganishi: www.jkt.mil.tz.

Ili kuangalia jina lako, fuata hatua hizi:

  • Ingiza jina la shule na namba ya shule uliyohitimu kidato cha sita mbele ya jina lako la shule.
  • Baada ya hapo, utaona sehemu iliyoandikwa “Waliochaguliwa”.
  • Bofya hapo kuona jina lako, kambi uliyopangiwa, mkoa na wilaya ya kambi husika.

Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 – Pakua PDF Hapa

Wito wa Mkuu wa JKT kwa Vijana

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele, ametoa wito kwa vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2025 kufika makambini kwa wakati ili kuungana na wenzao kujifunza stadi za kazi, stadi za maisha, uzalendo na utayari wa kulitumikia Taifa lao.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax, alipowasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26, alibainisha kuwa hadi kufikia mwaka huu wa 2025, JKT imeongeza uwezo wa kupokea vijana kutoka 40,000 mwaka 2021 hadi 60,000.

Hili limewezekana kupitia maboresho makubwa ya miundombinu ya makambi, lengo likiwa kuhakikisha wahitimu wote wa kidato cha sita wanapata nafasi ya mafunzo haya muhimu.

  1. Vitu vya Kwenda Navyo JKT Mujubu Wa Sheria 2025
  2. Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 Mujibu wa Sheria
  3. Ni Lini TAMISEMI Itatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026?
  4. Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026
  5. Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)
  6. Waliochaguliwa Kidato cha Tano Mkoa wa Dodoma 2025/2026
  7. Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano Dar es Salaam 2025/2026
  8. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo