Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Sherehe Kubwa ya Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara mara tatu mfululizo Yanga Sc (Timu ya Wananchi), Tarehe Muhimu, Matukio ya Kusisimua, na Bei za Tiketi
Wiki ya Mwananchi, inayojulikana pia kama Yanga Day, ni tukio maalum linalofanyika kila mwaka ili kuadhimisha kilele cha klabu ya Yanga ambapo utambulisho wa kikosi kipya cha wachezaji na benchi la ufundi hufanyika.
Mwaka huu, tukio hili limepangwa kufanyika tarehe 4 Agosti 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam. Hapa chini, tutakupa maelezo yote muhimu kuhusu tarehe, matukio, na bei za tiketi kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi 2024.
Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day) Tarehe & Mahali
Tarehe 4 Agosti 2024, katika Uwanja wa kimataifa wa Benjamin Mkapa utakuwa kitovu cha sherehe kuu ya Wananchi ambayo hujulikana kama Yanga Day 2024. Hii ni siku maalum ambapo klabu ya Yanga inakutanisha mashabiki wake kwa shamrashamra za aina yake, huku ikiwatambulisha nyota wapya watakaowakilisha klabu katika msimu ujao.
Utambulisho wa kikosi cha Yanga Sc kuelekea msimu wa 2024/2025 utaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na hatimaye mchezo wa kirafiki ambao utawafanya mashabiki wa Yanga SC kushuhudia kiwango cha kusakata kabumbu kutoka kwa kikosi kipya.
Matukio ya Kutarajia Yanga Day 2024
Wiki ya Mwananchi inajumuisha matukio mbalimbali yenye lengo la kutoa burudani na kuimarisha mshikamano kati ya klabu na mashabiki wake. Baadhi ya matukio yanayotarajiwa ni:
- Utambulisho wa Kikosi Kipya: Wachezaji wapya watawasilishwa mbele ya mashabiki kwa mara ya kwanza, wakiwa tayari kuonyesha uwezo wao uwanjani.
- Mechi ya Kirafiki: Timu ya Yanga itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu nyingine, ikitumika kama majaribio ya mwisho kabla ya kuanza kwa msimu rasmi.
- Burudani kutoka kwa Wasanii: Wasanii mbalimbali watapamba jukwaa, wakitoa burudani ya muziki na ngoma, kuhakikisha mashabiki wanafurahia kila dakika ya sherehe.
- Hotuba na Sherehe: Viongozi wa klabu watazungumza na mashabiki, kutoa mipango na malengo ya klabu kwa msimu ujao.
Bei za Tiketi za Wiki ya Mwananchi 2024 na Maeneo ya Kununua
Ili kuhakikisha kila shabiki anapata nafasi ya kushiriki katika sherehe hii, Yanga imeweka viwango tofauti vya tiketi:
- VIP A: Tsh 50,000
- VIP B: Tsh 30,000
- VIP C: Tsh 15,000
- Jukwaa la Machungwa: Tsh 10,000
- Mzunguko: Tsh 5,000
Tiketi za Royal
Pia kutakua na tiketi za Royal ambazo zitajumuisha vitu mbalimbali ikiwemo jezi, siti za kukaa VIP A, Huduma ya Chankula, Viburudisho na usafiri wa kwenda na kurudi.Tikite hizi zinapatikana kwa bei ya Tsh 300,000.
Wauzaji wa Tikiti za Yanga Day 2024
Tiketi za Yanga Day 2024 zinapatikana katika maeneo yafuatayo:
- Young Africans – Jangwani
- Vunja Bei – Kinondoni, Sinza, Mbeya
- T-Money Ltd – Kigamboni
- Gitano Samweli – Mbagala Zakiem
- Khalfan Mohamed – Ilala
- Kibacho Juma – Morogoro
- Mwanaidi Izina – Morogoro
- Godwin Fredy – Geita
- Twisty Investment – Geita
- Gwambina Lounge – Gwambina
- Karoshy Pamba – Dar Live (Zakhiem)
- Antonio Service – Sinza, Kivukoni
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- Sovereign – Kinondoni Makaburini
- View Blue Skyline – Mikocheni
- Mkaluka Traders – Machinga Complex
- New Tech General Traders – Ubungo
- Sabana Business – Mbagala Maji Matitu
- Juma Burrah – Mbeya
- Juma Burrah – Kivukoni
- Juma Burrah – Msimbazi
- Alphan Hinga – Ubungo
- Mtemba Service Co – Temeke
- Jackson Kimambo – Ubungo
- Shirima Shop – Leaders
- Lampard Electronics – DSM
Editor’s Picks:
Weka Komenti