Yanga SC vs Cosmopolitan Leo Saa Ngapi 18/02/2026

Yanga SC vs Cosmopolitan Leo Saa Ngapi 18/02/2026

Michuano ya kombe la shirikisho Tanzania, maarufu kama CRDB Federation Cup (zamani FA Cup), inaendelea kutimua vumbi leo Jumatano, tarehe 18 Februari 2026. Hii ni hatua muhimu ambapo vigogo wa soka nchini na timu zinazochipukia zinachuana vikali kuwania ubingwa na nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa. Miongoni mwa mechi zinazovuta hisia za mashabiki wengi ni Yanga SC vs Cosmopolitan Leo Saa Ngapi 18/02/2026, pambano la hatua ya 64 Bora linalotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Yanga SC vs Cosmopolitan Leo Saa Ngapi 18/02/2026?

Kwa mujibu wa ratiba rasmi ya CRDB Federation Cup, mchezo kati ya Yanga SC na Cosmopolitan FC utapigwa:

  • 📅 Jumatano, 18 Februari 2026
  • 🕐 Saa 1:00 Usiku
  • 🏟️ Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam

Huu ni mchezo wa hatua ya 64 Bora, ambapo mshindi atasonga mbele kuendelea na harakati za kutwaa taji la kombe hilo.

Yanga SC vs Cosmopolitan Leo Saa Ngapi 18/02/2026

Yanga Yarejea Michuno ya Ndani Baada ya CAF

Yanga SC wanaingia katika mchezo huu wakiwa wametoka kwenye kampeni ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Licha ya kuhitimisha hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 3–0 dhidi ya JS Kabylie katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, mabingwa hao wa Tanzania Bara hawakufanikiwa kufuzu robo fainali.

Walihitaji ushindi wa zaidi ya mabao matatu ili kujiweka katika nafasi ya kusonga mbele, lakini matokeo ya sare tasa kati ya AS FAR Rabat na Al Ahly yaliwahakikishia AS FAR kufuzu kwa alama tisa, huku Al Ahly wakiongoza kundi kwa alama 10.

Yanga walimaliza nafasi ya tatu kwa alama nane, na JS Kabylie wakishika mkia kwa alama tatu. Matokeo hayo yamefunga rasmi ukurasa wa michuano ya kimataifa kwa msimu huu, na sasa nguvu zote zimeelekezwa kwenye mashindano ya ndani.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba Yafuzu 32 Bora CRDB Federation Cup Baada ya Kuifunga Greenland 3-0
  2. Droo ya Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026
  3. Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025/2026
  4. Droo Robo Fainali CAF 2025/26: Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Kupangwa Leo Cairo
  5. CAF Yalaani Vurugu Mechi ya Al Ahly vs AS FAR Ligi ya Mabingwa Afrika 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo