Yanga Sc Wabeba Kombe la Toyota Cup 2024
Dar es Salaam, Tanzania – Katika mtanange uliofanyika Uwanja wa Toyota, Bloemfontein, Afrika Kusini, mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wameonyesha ubabe wa hali ya juu kwa kuwachapa Kaizer Chiefs mabao 4-0 na kunyakua kombe la Toyota Cup 2024.
Yanga SC, mabingwa wa Tanzania, walionyesha ubora wao tangu dakika za mwanzo za mchezo. Baada ya kushinda dhidi ya TS Galaxy kwa bao 1-0 siku ya Jumatano, Yanga SC walikuwa na ari ya kuendeleza ushindi huo dhidi ya Kaizer Chiefs.
Katika mchezo wa leo wa Toyota cup Dhidi ya Kaizer Chiefs, Mchezaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube, alifungua ukurasa wa mabao kwa Yanga SC katika dakika ya 25 baada ya kupokea pasi nzuri na kufunga goli la kwanza.
Hii iliwaweka Yanga SC katika nafasi nzuri ya kuendeleza shambulio lao dhidi ya Kaizer Chiefs.
Dakika chache baada ya goli la kwanza, mchezaji mahiri Aziz Ki aliwapa Yanga SC goli la pili. Kwa ustadi wake mkubwa, Ki alifunga goli hili baada ya kupokea pasi maridhawa na kufanikisha mpango wa mashambulizi ya Yanga SC.
Baada ya kipindi cha mapumziko, Yanga SC waliendelea kuonyesha makali yao. Katika dakika ya 57, Clement Mzize alifunga goli la tatu na kuwapa Yanga SC uongozi wa 3-0. Licha ya mabadiliko yaliyofanywa na timu zote, Yanga SC waliendelea kudhibiti mchezo na kushambulia kwa nguvu.
Katika dakika ya 63, Ki alikamilisha ushindi wa Yanga SC kwa kufunga goli lake la pili katika mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 4-0. Ushindi huu mkubwa uliwakatisha tamaa mashabiki wa Kaizer Chiefs ambao walikuwa na matarajio makubwa baada ya maandalizi ya muda mrefu.
Ushindi huu wa Yanga SC ni kielelezo cha maandalizi mazuri na ubora wa wachezaji wao. Huku wakiwa na malengo makubwa msimu ujao, ushindi huu unawaweka katika nafasi nzuri ya kuendeleza mafanikio yao kwenye ligi na mashindano ya kimataifa.
Kwa upande wa Kaizer Chiefs, matokeo haya ni pigo kubwa na yanaonyesha kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kuweza kushindana na timu kubwa kama Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates msimu ujao. Timu hiyo imekuwa na msimu mbaya, ikimaliza katika nafasi ya 10 kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), matokeo mabaya zaidi kuwahi kuyapata.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo 28/07/2024 – Toyota Cup
- Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 – Toyota Cup
- Matokeo Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki
- Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki
- Hizi Apa Picha Za Jezi Mpya Ya Yanga Sc 2024/2025
- PSL Betway Premiership Fixtures 2024/2025
- MTN8 Quarter Final Fixtures 2024/2025 Confirmed
Weka Komenti