Yanga VS Fountain Gate Leo 04/12/2025 Saa Ngapi?
Katika mwendelezo wa michezo ya NBC Premier League leo Alhamisi, mashabiki wa soka nchini wanatarajia pambano la kukatana shoka kati ya bingwa mtetezi wa ligi kuu Yanga SC na Fountain Gate. Mchezo huu, ambao umekuwa ukizungumziwa sana kutokana na maandalizi ya timu zote, utachezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.
Kulingana na ratiba rasmi, mchezo wa Yanga vs Fountain Gate leo tarehe 04/12/2025 utaanza saa 10:00 jioni, na mashabiki watapata fursa ya kuutazama mubashara kupitia AzamSports1HD.
Msimamo wa Timu na Uzito wa Mchezo
Yanga SC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imekusanya pointi 10. Wakati huo huo, wapinzani wao Fountain Gate wamekuwa wakionyesha kujiamini katika maandalizi waliyoyafanya kabla ya mchezo huu muhimu.
Huku timu zingine kama Simba SC na Mbeya City pia zikiendelea na ratiba zao, michezo ya Alhamisi imeibua msisimko mkubwa katika mbio za kusaka pointi tatu muhimu.
Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo
Fountain Gate: “Tumekuja kushindana ili kupata matokeo mazuri”
Kocha wa Fountain Gate, Mohammed Laizer, amesisitiza kuwa licha ya ubora wa Yanga, kikosi chake kipo tayari kupambana kikamilifu. Akinukuliwa akisema:
“Tuko tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga. Maandalizi yanaenda vizuri. Tunajua tunakutana na Yanga ambayo ni timu bora. Tunawaheshimu, lakini sisi tumekuja kushindana ili kupata matokeo mazuri.”
Kauli yake imeonyesha dhamira ya Fountain Gate kutafuta ushindi dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria, hasa wakitambua ukubwa wa mchezo wenyewe.
Yanga SC: “Tutacheza kama tunavyocheza Ligi ya Mabingwa”
Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Gonçalves, ameweka wazi kuwa maandalizi ya timu yake yamelenga kuhakikisha ushindi unapatikana bila kujali ukubwa wa mpinzani. Akinukuliwa akisema:
“Tunafahamu kuwa wapinzani wetu wamejiandaa vizuri pia. Tunaheshimu kila mpinzani anayekuja mbele yetu. Tutacheza kama vile tunacheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa. Falsafa yetu haitabadilika. Dhamira yetu ni ushindi tu.”
Kauli hii imeongeza ari kwa mashabiki wa Yanga ambao wanatarajia kuona kikosi chao kikicheza kwa kasi na nidhamu wanayoonyesha katika mechi kubwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo Wa Championship Ligi Daraja la Kwanza Tanzania 2025/2026
- Msimamo wa Kundi la Azam Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
- Simba Yachezea Kichapo cha Pili Mfululizo Makundi Klabu Bingwa
- Singida BS Yapata Pointi ya Kwanza Makundi Kombe la Shirikisho CAF
- Matokeo ya Stade Malien vs Simba leo 30/11/2025
- Kikosi cha Simba vs Stade Malien leo 30/11/2025
- Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 30/11/2025








Leave a Reply