Kikosi cha Simba Vs Tabora United Leo 18/08/2024 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Tabora United
Leo tarehe 18 Agosti 2024, klabu ya Simba SC itashuka dimbani kuikabili Tabora United katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/2025. Mechi hii itafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ikitarajiwa kuanza saa 10:15 jioni.
Mchezo huu unachukuliwa kwa uzito mkubwa na mashabiki wa Simba SC ambao wanamategemeo makubwa ya kuona timu yao ikianza msimu mpya kwa kishindo baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu mitatu mfululizo.
Kocha mpya wa Simba SC, Fadlu Davids kutoka Afrika Kusini, atakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha timu inarudisha makali yake kwa kurudi kwenye nafasi yake ya juu katika soka la Tanzania. Upande wa Tabora United, kocha Francis Kimanzi kutoka Kenya ataanza safari yake ya Ligi Kuu Tanzania akiwa na matumaini ya kufanya vizuri na kuleta changamoto mpya kwa vigogo wa soka la Tanzania.
Katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/2024, Simba SC ilimaliza nafasi ya tatu, nyuma ya Yanga SC na Azam FC, hali ambayo imeibua shauku kubwa ya mashabiki kuona mabadiliko makubwa msimu huu. Kocha Fadlu Davids ameanza kazi kwa bidii tangu kujiunga na klabu, akijaribu kurejesha hadhi ya timu kwa kufanya maandalizi ya nguvu ikiwa ni pamoja na kambi ya mazoezi nchini Misri.
Tabora United, ambayo inacheza msimu wake wa pili katika Ligi Kuu, imefanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake ili kujiimarisha zaidi. Msimu uliopita, timu hii ilinusurika kushuka daraja kwa mara ya pili kupitia mechi za mchujo. Katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Simba SC msimu uliopita, Tabora United ilipoteza zote, ikifungwa mabao 4-0 ugenini na 2-0 nyumbani. Hata hivyo, Tabora United imefanya usajili wa wachezaji wenye uzoefu na umakini mkubwa, wakilenga kuvunja rekodi hiyo mbovu leo.
Kikosi cha Simba Vs Tabora United Leo 18/08/2024
Simba SC imefanya maboresho makubwa sana kwenye kikosi chake kwa kusajili nyota kadhaa wapya wenye vipaji vya hali ya juu, akiwemo mshambuliaji hatari Leonal Ateba kutoka USM Alger ya Algeria, ambaye alijiunga na timu siku ya mwisho ya usajili. Ateba anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha Simba SC inaanza msimu vizuri.
Mbali na Ateba, wachezaji wapya kama vile Augustine Okejepha, Debora Mavambo, Joshua Mutale, na Jean Charles Ahoua nao wanatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika mechi hii. Kocha Fadlu Davids ameelezea matumaini yake kwa kikosi hiki kipya, akisisitiza umuhimu wa kupata pointi tatu katika mchezo wa leo ili kuanza msimu kwa ushindi.
Hapa chini tutakuletea kikosi rasmi cha Simba ambacho kitaanza dhidi ya Tabora United katika mchezo huu wa ligi. Kocha mkuu wa simba Fadlu Davids anatarajiwa kutangaza kikosi chake mida ya saa tisa leo, na tutaorozesha wachezaji wote watakao unda kikosi hapa.
Utabiri wa Kikosi cha Simba Vs Tabora United
Kwa kuangalia michezo iliopita na ubora walioonesha wachezaji mbalimmbali wa SImba, habariforum tunatarajia wekundu wa msimbazi wataanza na wachezaji wafuatao katika mchezo huu wa leo.
- 26 Camara
- 33 Kijili
- 15 Hussein C
- 14 Hamza
- 20 Che Malone
- 25 Okejepha
- Sinda
- 16 Karabaka
- 17 Fernandes
- 11 Mukwala
- 10 Ahoua
- 7 Mutale
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti