Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025 Saa Ngapi?

Yanga Vs Namungo FC Leo 13 05 2025 Saa Ngapi

Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025 Saa Ngapi?

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo tarehe 13 Mei 2025 watashuka dimbani kwa mara nyingine kuendelea na safari ya kutetea taji lao la ubingwa, ambapo watakutana uso kwa uso na Namungo FC ya kocha Juma Mgunda katika uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Kwa sasa, Yanga SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa alama 70, ikiwa ni matokeo ya msimu mzuri waliouonesha hadi sasa. Ushindi katika mchezo wa leo ni wa muhimu kwa Wananchi, kwani utawapa nafasi ya kuendelea kujihakikishia nafasi ya kwanza huku wakiendeleza presha kwa wapinzani wao wa karibu.

Namungo FC wanashika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 31. Timu hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa dhidi ya Yanga SC, hasa ikizingatiwa historia ya michezo ya hivi karibuni baina ya timu hizi mbili. Katika mechi tano za mwisho walizokutana, Namungo FC haijawahi kuibuka na ushindi hata mara moja.

Muda na Mahali pa Mchezo:

Mchezo huu wa Ligi Kuu ya NBC utafanyika katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, na utaanza saa 10:00 jioni. Mashabiki wanashauriwa kuwahi uwanjani mapema ili kushuhudia burudani ya kandanda la hali ya juu kutoka kwa mabingwa watetezi.

Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025 Saa Ngapi?

Takwimu za Mechi Tano Zilizopita: Yanga Vs Namungo

Katika michezo mitano ya mwisho kati ya Yanga SC na Namungo FC:

  • Namungo FC 0-2 Yanga SC
  • Namungo FC 1-3 Yanga SC
  • Yanga SC 1-0 Namungo FC
  • Yanga SC 2-0 Namungo FC
  • Namungo FC 0-2 Yanga SC

Kwa ujumla, Yanga SC imeshinda mechi zote 5, ikifunga jumla ya mabao 9 huku ikiruhusu mabao 2 pekee. Rekodi hii inaonesha ubora mkubwa wa Wananchi dhidi ya Namungo na itaongeza presha kwa wageni hao leo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba Sc vs KMC leo 11 May 2025 Saa Ngapi?
  2. Simba Yapewa Vitisho Vikali na KMC Kuelekea Mechi ya Kesho Mei 11, 2025
  3. Napoli Yajipanga Kumsajili Jack Grealish Kutoka Man City
  4. KENGOLD Yapanga Kuipeleka Simba Ruvuma Juni 18
  5. Simba SC Yakata Tiketi Ligi ya Mabingwa Afrika 2025-2026 Baada ya Kufikisha Pointi 66
  6. Yanga Yashikilia Msimamo wa Kutocheza Dabi Licha Ya Majibu ya CAS
  7. Simba Yaitandika JKT na Kujiweka Kwenye Njia ya Ligi ya Mabingwa
  8. Matokeo JKT Tanzania vs Simba Leo 05/05/2025
  9. Sababu 3 Zilizofanya CAS Kuitupilia Mbali Kesi ya Yanga
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo