Zimamoto VS Yanga Leo 29/04/2025 Saa Ngapi?

Matokeo ya Zimamoto VS Yanga Leo 29 04 2025

Zimamoto VS Yanga Leo 29/04/2025 Saa Ngapi?

Kikosi cha Young Africans SC (Yanga) kinatarajiwa kurejea tena Uwanja wa Gombani, Pemba usiku wa leo kwa ajili ya kuikabili Zimamoto FC katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Muungano. Mchezo huo unatajwa kuwa wa kihistoria, ukiendelea kufufua hadhi ya mashindano hayo yaliyorejeshwa rasmi mwaka 2024 baada ya kusimama kwa zaidi ya miongo miwili tangu mwaka 2003.

Saa Ngapi Mechi Itaanza?

Kwa mujibu wa ratiba rasmi, pambano kati ya Zimamoto FC dhidi ya Yanga SC litapigwa leo Jumanne, tarehe 29 Aprili 2025, kuanzia saa 1:15 usiku katika uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba. Hii ni nusu fainali ya pili, ikifuatia ile iliyochezwa jana kati ya JKU na Azam FC.

🔰Taarifa Kamili Kuhusu Mechi ya Zimamoto Vs Yanga🔰

  • 🏆 #MuunganoCupSemiFinal
  • ⚽️ Zimamoto FC🆚Young Africans SC
  • 📆 29.04.2025
  • 🏟 Gombani, Pemba
  • 🕖 01:15 Usiku

Zimamoto VS Yanga Leo 29/04/2025 Saa Ngapi?

Yanga SC: Kuongeza Rekodi ya Kombe la Muungano

Yanga, ambayo inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi 70 baada ya mechi 26, inaingia kwenye mechi hii ikiwa na kiu ya kurejea Dar es Salaam na kombe mkononi. Hadi sasa, Yanga imefanikiwa kulibeba Kombe la Muungano mara sita, sawa na Simba SC, hivyo ushindi kwenye mashindano ya mwaka huu unaweza kuwa nafasi ya kuandika historia kwa kulibeba taji hilo kwa mara ya saba.

Tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 1982, Yanga ilibeba taji hilo miaka ya 1983, 1987, 1991, 1996, 1997 na 2000. Kwa upande mwingine, Simba ambao ni mabingwa watetezi, walilitwaa taji hilo kwa mara ya sita mwaka jana (2024) baada ya kuifunga Azam FC 1-0 kwenye fainali iliyopigwa Aprili 27, kupitia bao la Babacar Sarr dakika ya 77.

Zimamoto FC: Kusaka Historia Mpya

Zimamoto FC, inayonolewa na kocha Mohamed Ali, inakamata nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar ikiwa na pointi 36 baada ya mechi 22. Kikosi hicho kinajivunia ushindi wake wa hatua ya robo fainali dhidi ya Coastal Union kwa bao 1-0, matokeo yanayowapa morali kubwa kuelekea pambano la leo. Kwa upande wao, Yanga waliichapa KVZ mabao 2-0 kwenye robo fainali, na wanaingia nusu fainali hii wakiwa na matumaini makubwa ya kuendelea na mwenendo mzuri.

Zimamoto haijawahi kutwaa Kombe la Muungano tangu kuanzishwa kwake, na kwa kushinda leo dhidi ya moja ya vigogo wa soka Tanzania, itaweka historia mpya. Timu pekee kutoka Zanzibar zilizowahi kutwaa kombe hilo ni Malindi (1989, 1992) na KMKM (1984).

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Zimamoto VS Yanga Leo 29/04/2025
  2. Ratiba ya Kombe la Muungano 2025
  3. Liverpool Wafanikiwa Kuwa Mabingwa EPL 2024/2025
  4. Ratiba ya Fainali Kombe La Shirikisho Afrika CAF 2024/2025
  5. Simba SC Yatinga Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Baada ya Sare na Stellenbosch
  6. Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo