Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2025/2026 (Selection Vyuo Vya Kati)

Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2025/2026 (Selection Vyuo Vya Kati)

Wahitimu wengi wa elimu ya sekondari ngazi ya kidato cha nne nchini Tanzania huwa na ndoto mbalimbali kuhusu mustakabali wa maisha yao baada ya mitihani ya taifa. Ili kutambua na kukuza ndoto hizi, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, imeweka njia mbalimbali zinazomsaidia mwanafunzi kuchagua mwelekeo wa maisha yake ya kitaaluma kulingana na uwezo na matamanio aliyo nayo.

Njia hizi mbili kuu ni kuendelea na elimu ya kidato cha tano au kujiunga na vyuo vya kati. Wakati baadhi ya wanafunzi wanachagua njia ya kidato cha tano kwa lengo la kufikia elimu ya juu na shahada, si wote wanaofaulu kupata alama zinazokidhi vigezo vya kuchaguliwa. Hapo ndipo umuhimu wa vyuo vya kati unapojitokeza—njia mbadala yenye nafasi pana, isiyohitaji ufaulu wa hali ya juu kulinganisha na njia ya kidato cha Tano lakini inayoandaa wataalamu wa fani mbalimbali kwa soko la ajira la ndani na nje ya nchi.

Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2025/2026 kwa Mikoa ya Tanzania

Vyuo vya Kati: Nguzo ya Maendeleo kwa Vijana wa Tanzania

Vyuo vya kati vya serikali ni taasisi muhimu zinazotoa elimu ya ufundi na stadi mbalimbali kama vile afya, TEHAMA, kilimo, ualimu, biashara na fani nyingine nyingi kwa vijana walikidhi vigezo. Mafunzo yanayotolewa husaidia kujenga ujuzi wa vitendo kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita, hivyo kuwaandaa vyema kwa maisha ya kazi au ujasiriamali.

Kupitia zoezi rasmi la TAMISEMI Selection 2025/2026, wanafunzi waliohitimu kidato cha nne huchaguliwa kwa umakini na kuwekwa kwenye vyuo vya kati kulingana na ufaulu wao, matakwa yao ya fani, pamoja na nafasi zilizopo katika vyuo mbalimbali nchini.

Mchakato wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya kati kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 unaratibiwa kwa weledi na uwazi mkubwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Hii ni hatua muhimu inayoweka msingi wa maisha ya kitaaluma na ajira kwa wahitimu wa kidato cha nne. Kwa wale waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha tano au walioamua mapema kuchukua mkondo wa taaluma ya vitendo, majina ya waliochaguliwa vyuo vya kati 2025/2026 huwa ni habari inayosubiriwa kwa hamu.

Kwao hii ni fursa ya pekee kwao kupata elimu ya kati inayozingatia ujuzi unaohitajika moja kwa moja katika sekta mbalimbali za ajira.

Ni Lini Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2025/2026 Yatatangazwa?

Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, Ofisi ya Rais – TAMISEMI huanza mchakato wa upangaji wa wanafunzi katika shule na vyuo. Kwa kawaida, orodha ya majina ya waliochaguliwa vyuo vya kati 2025/2026 hutangazwa rasmi kuanzia mwezi Juni 2025, ikifuatiwa na mizunguko mingine ya uteuzi kama itahitajika.

Ni muhimu kwa wanafunzi na wazazi kufuatilia tovuti rasmi ya TAMISEMI ili kupata taarifa za haraka na sahihi kuhusu uchaguzi huu.

Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Vyuo vya Kati 2025/2026

Ili kuona kama umechaguliwa kujiunga na chuo cha kati kwa mwaka wa masomo 2025/2026, fuata hatua hizi:

  1. Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI kupitia kiungo: https://selform.tamisemi.go.tz
  2. Bofya kipengele cha “Selection Results”
  3. Chagua mkoa na wilaya ulipofanya mtihani wa kidato cha nne.
  4. Tafuta jina la shule yako ya sekondari na uangalie majina ya wanafunzi waliochaguliwa kutoka shule hiyo.
  5. Tafuta jina lako kwenye orodha na ujue chuo pamoja na kozi uliyopangiwa.

Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Vyuo vya Kati kwa Kila Mkoa 2025/2026

Ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wanafunzi na wazazi, tumeandaa jedwali lifuatalo likiwa na majina ya mikoa yote ya Tanzania Bara. Bonyeza jina la mkoa ili kufunguka ukurasa wenye wilaya zake na hatimaye kuona majina ya waliochaguliwa vyuo vya kati kwa mwaka wa masomo 2025/2026:

MKOA MKOA MKOA
ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

Kumbuka: Kiungo cha kila mkoa kitakupeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wa TAMISEMI wenye orodha ya wilaya za mkoa huo mara baada ya majina hayo kutangazwa. Bonyeza jina la wilaya yako ili kuona wanafunzi waliopangiwa vyuo vya kati.

Vigezo Vinavyotumika Kuchagua Waliojiunga na Vyuo vya Kati

Serikali hutumia vigezo maalum kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kwenda vyuo vya kati wanakidhi mahitaji ya kozi husika. Baadhi ya vigezo hivyo ni:

  1. Ufaulu wa jumla katika masomo ya kidato cha nne – hasa kwa masomo yanayohusiana na kozi aliyoomba mwanafunzi.
  2. Chaguo la mwanafunzi alipokuwa anajaza fomu ya Selform.
  3. Upatikanaji wa nafasi katika chuo na kozi husika.
  4. Uwiano wa kijinsia na muktadha wa kijiografia kwa kuzingatia usawa wa fursa.

Nini Kinafuata Baada ya Kuchaguliwa?

Mwanafunzi akishajua chuo alichopangiwa, anapaswa:

  • Kupakua na kuchapisha barua ya kupokelewa chuoni ambayo hujulikana kama (Joining Instruction).
  • Kujiandaa na mahitaji muhimu ya chuo kama ada, vifaa vya masomo, na makazi.
  • Kuhakikisha anaripoti chuoni kwa tarehe iliyopangwa rasmi na TAMISEMI au uongozi wa chuo husika.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tarehe ya Kutangazwa Selection Za Kidato cha Tano 2025
  2. Waliochaguliwa Kidato Cha Tano na Vyuo vya Kati 2025 (Tamisemi Selection)
  3. Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)
  4. Tarehe ya Kuripoti Makambini JKT Mujibu wa Sheria 2025
  5. Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 Mujibu wa Sheria
  6. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Jeshi la Polisi 2025
  7. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2025/2026
  8. Vitu vya Kwenda Navyo JKT Mujibu Wa Sheria 2025
  9. Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo