Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024 | Kikosi cha Yanga leo dhidi ya CBE SA | Kikosi cha Yanga Leo CAF

Leo, tarehe 21 Septemba 2024, macho ya wapenzi wa soka nchini Tanzania na kwingineko barani Afrika yatakuwa yakielekezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, ambapo Yanga itakutana na CBE ya Ethiopia kwenye mechi ya marudiano ya kuwania nafasi katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mechi hii ni muhimu kwa Yanga kwani itahitimisha safari yao kuelekea hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa. Timu ya Yanga, ambayo tayari imeshinda kwa bao 1-0 katika mechi ya awali iliyochezwa jijini Addis Ababa, Ethiopia, inahitaji sare au ushindi wowote ili kufuzu. Hata hivyo, wachezaji wa Yanga wameweka wazi kwamba wanataka kuonyesha uwezo wao zaidi kwa kuondoka na ushindi wa mabao mengi.

Dickson Job, nahodha msaidizi wa Yanga, alisema: “Kila mmoja wetu anaitaka mechi hii kwa nguvu, tunataka ushindi mkubwa na kuridhisha mashabiki wetu waliotupa sapoti kubwa sana.” Maneno haya yanadhihirisha azma ya Yanga kurudisha heshima kwa mashabiki wao, hasa baada ya kushinda kwa ushindi mwembamba wa 1-0 kwenye mechi ya kwanza, ambapo walikosa nafasi nyingi za kufunga.

Yanga imekuwa na rekodi nzuri dhidi ya timu za Ethiopia katika michuano ya CAF. Katika mara nne ambazo wamekutana na timu za nchi hiyo, Yanga imewatoa wapinzani mara tatu, huku timu za Ethiopia zikishinda mara moja tu. Rekodi hii inatoa matumaini kwa Yanga, hasa ikizingatiwa ushindi wao wa 5-0 dhidi ya Saint-George mwaka 1969 na ushindi mwingine mkubwa wa 6-1 dhidi ya Coffee FC mwaka 1998.

Katika mechi ya leo, Yanga imejipanga kuhakikisha wanatengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga na kugeuza mechi hii kuwa ya kipekee. Kocha wao, Miguel Gamondi, ameweka wazi kwamba timu yake imejipanga vizuri. Alisema:
“Tumefanya maandalizi maalum kuhakikisha tunaitumia kila nafasi tutakayopata. Tumewasoma vizuri wapinzani wetu, tunaiheshimu CBE lakini tunahitaji kushinda nyumbani na kwa mabao mengi.”

Mazoezi ya Yanga kwa siku za hivi karibuni yamejikita kwenye kuboresha uwezo wa kufunga mabao, si kwa washambuliaji pekee bali pia kwa viungo na mabeki. Mbinu hii inalenga kuongeza uwezekano wa kufunga mabao mengi, jambo ambalo limekuwa tatizo kwa Yanga kwenye mechi za hivi karibuni.

Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

Kocha wa Yanga Miguel Gamond anatarajiwa kutangaza kikosi cha yanga kitakacho anza leo dhidi ya CBE majira ya saa moja usiku. Hapa tutakuletea orodha ya wachezaji wote watakao unda kikosi cha yanga leo dhidi ya CBE.

  • 39 Diarra
  • 21 Yao
  • 23 Boka
  • 5 Job
  • 4 Bacca
  • 20 Mkude
  • 9 Maxi
  • 27 Mudathir
  • 24 Muleke
  • 10 Moloko
  • 17 Chama
  • 25 Pacome

SUBS: Mshery, Kibabage, Aziz A, Nkane, Abuya, Aucho, Aziz Ki, Musonda, Dube

Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

Changamoto za CBE

CBE, licha ya kuwa timu changa kwenye michuano ya CAF, imeonyesha ushindani mkubwa. Katika raundi iliyopita walifanikiwa kuitoa SC Villa ya Uganda kwa jumla ya mabao 3-2. Ushindi wao wa ugenini wa 2-1 dhidi ya SC Villa ni ishara kwamba wanajua jinsi ya kucheza na timu kubwa ugenini, na hii inaiweka Yanga kwenye tahadhari kubwa.

Kocha wa CBE, Sisay Kumbe, alisema kuwa timu yake iko tayari kwa changamoto ya marudiano dhidi ya Yanga:
“Tunajua tunakutana na timu yenye wachezaji wazoefu, lakini tumejifunza mengi kutoka kwenye mechi ya kwanza. Hii haitakuwa mechi rahisi, lakini tutapambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.”

CBE ilitua Zanzibar mapema wiki hii kwa maandalizi makini ya mechi ya leo. Lengo lao kuu ni kupata ushindi wa mabao 2-0 au zaidi ili kufuzu moja kwa moja, au angalau kulazimisha sare ili mechi hiyo iishe kwa mikwaju ya penalti.

Mwamuzi wa Mechi Yanga Vs CBE SA

Mechi ya leo itaamuliwa na mwamuzi Abdel Aziz Bouh kutoka Mauritania, ambaye amekuwa sehemu ya mechi tatu zilizopita za Yanga katika michuano ya CAF. Rekodi ya Bouh na Yanga inaonesha kuwa Yanga imekuwa na bahati nzuri chini ya uamuzi wake, ikiwemo ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2023.

Tambo za Mashabiki wa Yanga Kuelekea Mchezo huu

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
  2. Yanga Vs CBE SA Leo 21/09/2024 Saa Ngapi
  3. Juma Mgunda Anukia KenGold Fc
  4. Yanga Yafika Zanzibar Tayari kwa Mchezo Dhidi ya CBE
  5. NMB Yaungana na Yanga Kuelekea Ligi ya Mabingwa Afrika
  6. Gamondi Aweka Wazi Nia Yake ya Kutwaa Ubingwa wa Afrika
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo