Ratiba ya Mechi za Leo 16/08/2025 CHAN
Michuano ya African Nations Championship (CHAN) 2024/2025, inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani pekee barani Afrika, inaendelea leo Jumamosi, tarehe 16 Agosti 2025, katika viwanja mbalimbali vya Afrika Mashariki.
Mashindano haya mwaka huu yanachezwa kwa mfumo wa ushirikiano wa mataifa matatu Kenya, Tanzania na Uganda, hali ambayo imeongeza msisimko mkubwa kwa mashabiki wa soka barani.Β CHAN imekuwa ni jukwaa muhimu kwa wachezaji wa ndani kuonyesha uwezo wao, huku mashabiki wakifurika viwanjani kushuhudia vipaji vipya vinavyoibuka. Leo, macho ya mashabiki yataelekezwa zaidi kwenye hatua ya mwisho ya mechi za makundi, hasa kundi B ambalo linakamilisha safari yake ya awali.
Ratiba ya Mechi za Leo 16/08/2025 CHAN
Tanzania vs Afrika ya Kati
- π Saa: 2:00 Usiku
- π Uwanja: Benjamin Mkapa Stadium β Dar es Salaam
- πΊ Mubashara: Azam Sports 1 HD
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars B) tayari imejihakikishia nafasi ya kufuzu kwa robo fainali. Hata hivyo, leo wanakamilisha hatua ya makundi kwa kukipiga dhidi ya Afrika ya Kati. Mashabiki wa nyumbani wanatarajia kuona mwendelezo wa matokeo mazuri, huku wachezaji wakipata nafasi ya kujiimarisha zaidi kabla ya hatua inayofuata.
Burkina Faso vs Madagascar
- π Saa: 2:00 Usiku
- π Uwanja: Amaan Stadium β Zanzibar
- πΊ Mubashara: Azam Sports 4 HD
Mechi nyingine ya kukukatana shoka itakayotimua vumbi leo ni kati ya Burkina Faso na Madagascar. Burkina Faso inaingia uwanjani ikiwa na alama 3, wakati Madagascar wakiwa na alama 4. Hii ni mechi ya uamuzi kwa pande zote mbili, kwani ushindi au sare unaweza kubadilisha mwelekeo wa nani ataungana na Tanzania kuingia robo fainali kutoka kundi hili.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Sifa za Kujiunga na Jeshi la Magereza Tanzania 2025
- Rayon Sports vs Yanga Leo 15/08/2025 Saa Ngapi?
- Kikosi cha Yanga vs Rayon Sports Leo 15/08/2025 Mechi ya Kirafiki
- Matokeo ya CHAN 2025 Kundi La Tanzania (Kundi B)
- Azam FC Yamwaga Mamilioni Ili Kumbakiza Nyota Wake Fei Toto
- Ratiba ya Mechi za Leo 14/08/2025 CHAN
- Ifahamu Gaborone United Wapinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa CAF 2025/2026
Leave a Reply