Simba SC Kuzindua Rasmi Jezi Mpya 2025/2026 Agosti 27

Simba SC Kuzindua Rasmi Jezi Mpya 2025/2026 Agosti 27

Wekundu wa Msimbazi Simba wametangaza rasmi kuwa uzinduzi wa jezi mpya za msimu wa 2025/2026 utafanyika Agosti 27, katika hafla maalumu itakayokuwa ya kipekee na yenye hadhi ya juu. Uzinduzi huo, ambao utahusisha wadhamini wapya wa jezi JayRutty Investment East Africa Ltd kwa kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya Diadora, unatajwa kuwa tukio la kihistoria litakaloweka alama kubwa katika klabu hiyo kongwe barani Afrika.

Simba SC Kuzindua Rasmi Jezi Mpya 2025/2026 Agosti 27

Tarehe na Mahali pa Uzinduzi

Shughuli ya uzinduzi itafanyika Jumatano, tarehe 27 Agosti 2025 kuanzia saa 1:00 usiku katika ukumbi wa kisasa wa Super Dome uliopo Masaki, Dar es Salaam. Simba SC imesisitiza kuwa tukio hilo halitakuwa la kawaida, bali litafanyika kwa upekee na ubora unaolingana na hadhi ya klabu hiyo na mashabiki wake. Kwa msimu wa 2025/2026, Simba SC imezindua jezi tatu tofauti ambazo zimetengenezwa nchini Italia kwa ushirikiano wa karibu kati ya JayRutty na Diadora. Jezi hizi zitatambulika kwa nembo za wadhamini hao na zimeelezwa kuwa za kiwango cha juu kisichowahi kuonekana katika soka la Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa klabu, Ahmed Ally, jezi hizo zimetengenezwa kwa ubunifu wa kipekee kiasi kwamba hata Diadora wenyewe walishangazwa na ubora wake.

Mashabiki wanatarajiwa kununua jezi kwa bei ya Tsh. 45,000 baada ya kuzinduliwa rasmi. Aidha, mchakato wa pre-order tayari unaendelea kupitia JayRutty Investment East Africa Ltd, pekee wenye mamlaka ya kuchukua maombi ya awali ya jezi hizi.

Tiketi na Faida za Washiriki

Kwa wale watakaohudhuria hafla ya uzinduzi wa jezi mpya za Simba SC, tiketi maalumu zinapatikana kwa gharama ya Tsh. 250,000. Ada hii itawawezesha mashabiki kushuhudia uzinduzi, kushiriki katika sherehe ya kipekee na kupokea jezi zote tatu za msimu mpya papo hapo ukumbini. Pia, wahudhuriaji watapata burudani ya moja kwa moja kutoka kwa wasanii wa muziki, live band, pamoja na huduma ya vyakula na vinywaji vya kutosha. Zaidi ya hayo, kutakuwa na mgeni rasmi ambaye ni gwiji wa zamani wa soka barani Afrika, anayejulikana duniani kwa mchango wake mkubwa katika mchezo wa mpira wa miguu, atakayefanikisha utambulisho wa jezi kwa mara ya kwanza.

Usambazaji wa Jezi Nchini

Mara baada ya uzinduzi huo, jezi za Simba SC zitapatikana katika maduka mbalimbali kote nchini Tanzania, ambayo tayari yameweka oda. Hii inahakikisha kuwa mashabiki na wapenzi wa soka kote nchini wanapata nafasi ya kuwa miongoni mwa wa kwanza kuvaa jezi mpya za msimu wa 2025/2026.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Jezi Mpya za Yanga 2025/2026 Zaanza Kuuzwa kwa Pre-Order – Fahamu Bei na Upatikanaji
  2. Ratiba ya Ngao ya Jamii 2025/2026
  3. Msimamo wa Ligi Kuu England EPL 2025/2026
  4. Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025 | Mechi za Robo fainali CHANI
  5. Timu zilizofuzu Robo Fainali CHAN 2024
  6. Man United Yaanza Safari ya EPL 2025/26 kwa Kupoteza Dhidi ya Arsenal
  7. Taifa Stars Kukutana na Morocco Robo Fainali ya CHAN 2025
  8. Madagascar Yatinga Robo Fainali Baada ya Ushindi wa 2-1 Dhidi ya Burkina Faso
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo