Bei ya Jezi Mpya za Yanga 2025/2026

Bei ya Jezi Mpya za Yanga 2025/2026

Timu ya Wananchi Yanga imethibitisha rasmi kuwa Jumapili, Agosti 24, 2025, ndiyo siku ambayo itatambulisha rasmi Jezi Mpya za Yanga 2025/2026 na kuanza kuziuza mara moja. Uzinduzi huu mkubwa utahusisha muonekano wa jezi zote tatu mpya za Yanga jezi ya nyumbani, ugenini, na jezi ya tatu ikiwa ni sehemu ya maandalizi makubwa kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, uzinduzi huo utaanza saa 6:00 mchana na utafanyika kwa njia ya kimtandao ili kuhakikisha mashabiki wote wa Yanga ndani na nje ya nchi wanapata nafasi ya kushuhudia tukio hilo muhimu. “Baada ya kuzindua tutaanza kuuza. Kauli mbiu yetu inasema tunazindua, tunauza,” alisema Kamwe.

Bei ya Jezi Mpya za Yanga 2025/2026

Mashabiki wote wa Yanga watapata nafasi ya kununua jezi mpya mara baada ya uzinduzi kukamilika.

Bei ya Jezi Mpya za Yanga 2025/2026 kwa rejareja imetajwa kuwa Tsh 45,000. Hii ni bei rasmi iliyowekwa na klabu kwa mashabiki wote wanaotamani kuvaa jezi za ubora wa juu za msimu mpya. Ni muhimu kutambua kuwa Yanga imeamua kufanya uzinduzi huu mapema zaidi kabla ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC, ambao jezi zao mpya zinatarajiwa kuzinduliwa Agosti 27, 2025. Hatua hii imewapa mashabiki wa Yanga nafasi ya kuwa wa kwanza kununua jezi za timu yao kabla ya msimu kuanza.

Bei ya Jezi Mpya za Yanga 2025/2026

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Jezi Mpya za Yanga 2025/2026 | Picha za Jezi Mpya za Yanga
  2. Matokeo ya Taifa Stars vs Morocco Leo 22/08/2025 CHAN
  3. Kikosi cha Taifa Stars vs Morocco Leo 22/08/2025 CHAN
  4. Cv ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026
  5. Wafungaji Bora CHAN 2025
  6. Jonathan Sowah Kuikosa Simba vs Yanga Ngao ya Jamii Septemba 16, 2025
  7. Sherehe za Wiki ya Mwananchi 2025 Yanga Day Kufanyika Benjamin Mkapa Septemba 12
  8. Khalid Aucho Asaini Mkataba wa Miaka 2 na Singida Black Stars
  9. Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025 | Mechi za Robo fainali CHANI
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo