Kikosi cha Yanga vs Wiliete Sc Leo 19/09/2025 | Kikosi cha Yanga leo dhidi ya Wiliete Sc
Kikosi cha Yanga vs Wiliete Sc Leo 19/09/2025
Hatimaye pazia la mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu barani Afrika linatarajiwa kufunguliwa rasmi leo Ijumaa, tarehe 19 Septemba 2025, ambapo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Yanga SC watashuka dimbani kuanza safari yao ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).
Wananchi wanakabiliwa na mtihani wa kwanza dhidi ya Wiliete Sports Clube kutoka Angola, mchezo unaopigwa katika Uwanja wa Estádio Nacional de Ombaka, Benguela, kuanzia saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Wiliete SC vs Yanga SC – Mechi ya Raundi ya Awali
Mchezo huu ni sehemu ya raundi ya awali ya michuano ya CAF Champions League 2025.
- Uwanja: Estádio Nacional de Ombaka, Benguela – wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 35,000.
- Timu pinzani: Wiliete Sports Clube (Angola).
- Tarehe: 19/09/2025.
- Muda: Saa 12:00 jioni EAT.
- Matangazo: AzamSports1HD.
Kwa upande wa Wiliete SC, hii ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kumaliza msimu wa 2024/2025 katika nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Angola (Girabola). Klabu hii ilianzishwa mwaka 2018, na kwa muda mfupi imeonyesha kasi kubwa ya ukuaji.
Kwa upande wa Yanga SC, uzoefu wao katika mashindano ya CAF unawapa faida kubwa. Katika misimu miwili iliyopita, Wananchi walitinga hatua za juu, ikiwemo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Safari hii wanataka kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ugenini kabla ya kurudi Tanzania kwa mechi ya marudiano.
Kikosi cha Yanga vs Wiliete SC Leo 19/09/2025
Kuelekea mchezo huu muhimu, macho ya mashabiki wote yapo kwenye orodha ya wachezaji wa Yanga SC watakaopangwa kuanza dhidi ya Wiliete SC. Hata hivyo, kama ilivyo desturi ya mashindano makubwa ya CAF, benchi la ufundi la Yanga litatangaza kikosi rasmi saa moja kabla ya mpira kuanza. Hapa Habariforum tutakuletea kikosi cha Yanga vs Wiliete SC Leo 19/09/2025 mara tu kitakapowekwa wazi rasmi na benchi la ufundi.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply