Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, leo itashuka dimbani katika uwanja wa Amaan, Zanzibar, kuikabili timu ya taifa ya Zambia katika mchezo muhimu wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026. Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 4 usiku na unatarajiwa kuvutia hisia kubwa kutoka kwa mashabiki wa soka nchini kutokana na umuhimu wake katika mbio za kufuzu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na benchi la ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na Kocha Hemed “Morocco” Suleiman, kikosi cha leo kimepangwa kwa umakini mkubwa, kikiwa na uwiano wa wachezaji wenye uzoefu na nyota wapya waliopata nafasi ya kuonesha uwezo wao. Hata hivyo, kocha huyo amekiri kuwa kikosi hicho kinakabiliwa na changamoto ya majeruhi kwa baadhi ya wachezaji wake muhimu.

“Tunakosa huduma za beki wetu wa kati, Dickson Job, ambaye ameumia misuli ya paja (hamstring),” alisema Kocha Hemed Morocco. “Ni pigo kwetu, lakini tuna wachezaji wengine ndani ya kikosi wanaoweza kujaza nafasi hiyo na kuendelea na mpango wetu wa kimkakati.”

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

Kikosi cha Taifa Stars Dhidi ya Zambia Leo Oktoba 8, 2025

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

Katika orodha rasmi iliyotangazwa kuitwa kwenye kambi maalumu ya maandalizi, Taifa Stars imejumuisha jumla ya wachezaji 26, ikiwemo makipa watatu, mabeki kumi, viungo saba na washambuliaji sita. Wachezaji wa safu ya ulinzi wameitwa kwa idadi kubwa kulinganisha na nafasi nyingine, ishara ya nia ya benchi la ufundi kuimarisha ukuta wa timu hiyo dhidi ya wapinzani wao wenye nguvu, Zambia.

Makipa

  • Yakoub Suleiman
  • Hussein Masalanga
  • Zuberi Foba

Mabeki

  • Lusajo Mwaikenda
  • Bakari Mwamnyeto
  • Lameck Lawi
  • Miano Danilo
  • Haji Mnoga
  • Wilson Nangu
  • Pascal Msindo
  • Ibrahim Abdulla
  • Novatus Dismas

Viungo

  • Aziz Andabwile
  • Yahya Zayd
  • Yusuph Kagoma
  • Feisal Salum
  • Halid Habibu
  • Habibu Idd
  • Morice Abraham

Washambuliaji

  • Charles Mmombwa
  • Suleiman Mwalimu
  • Edwin Balua
  • Offen Chikola
  • Tarryn Allarakhia

Kati ya wachezaji walioitwa, baadhi yao ni nyota waliokuwa hawajaitwa kwa muda mrefu kwenye timu ya taifa, wakiwemo Haji Mnoga, Miano Danilo, Offen Chikola, Habibu Khalid, Aziz Andabwile, Tarryn Allarakhia na Edwin Balua. Urejeo wa nyota hawa unatarajiwa kuongeza ushindani na chachu mpya katika kikosi cha leo.

Hata hivyo, wachezaji kadhaa waandamizi kama Aishi Manula, Mbwana Samatta, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein na Simon Msuva hawajahumishwa katika kikosi hiki cha sasa, jambo lililoshangaza baadhi ya wadau wa soka lakini likitajwa kuwa ni sehemu ya mpango wa mabadiliko ndani ya timu. Pia, beki wa Simba Abdulrazack Hamza na kiungo wa KMC Ahmed Pipino hawajaitwa kutokana na majeraha na sababu za kiufundi.

Umuhimu wa Mchezo wa Leo

Mchezo wa leo dhidi ya Zambia ni wa mwisho kwa Taifa Stars katika kundi E la kufuzu Kombe la Dunia 2026. Tanzania inahitaji ushindi ili kufikisha pointi 13, hatua itakayoweka timu hiyo katika nafasi ya pili nyuma ya vinara Morocco.

Kumaliza katika nafasi ya pili kutaiweka Taifa Stars katika nafasi nzuri ya kuwania moja ya nafasi nne za ziada za hatua ya mchujo (playoffs) kwa timu za Afrika, zitakazopigania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika nchini Canada, Mexico na Marekani.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Djigui Diarra Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba 2025/2026
  2. Ahmad Ali Ashinda Tuzo ya Kocha Bora Mwezi Septemba 2025/2026
  3. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  4. Cv ya Dimitar Pantev Kocha Mpya wa Simba Sc 2025
  5. Singida BS Yaendeleza Ubabe Mbele ya Mashujaa na Kubaki Kinara wa Ligi Kuu Bara
  6. Ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  7. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo