Sifa za Kujiunga na JKT 2024, Mafunzo ya Kujitolea | Vigezo vya Kujiunga na Mafunzo ya Kujitolea JKT 2024/2025
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza rasmi nafasi za kujiunga na mafunzo ya kujitolea kwa mwaka 2024. Tangazo hilo limetolewa septemba 25 na vijana wote wenye sifa wameombwa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya nafasi hizi.
Mafunzo haya ni fursa ya kipekee kwa vijana wa Tanzania Bara na Visiwani, ambao wanataka kupata ujuzi, uzalendo, na kujiimarisha katika maisha ya baadaye. Katika makala hii, tutajadili sifa zinazohitajika kwa ajili ya kujiunga na JKT kwa mwaka 2024, utaratibu wa maombi, pamoja na vifaa muhimu ambavyo vijana wanatakiwa kuwa navyo kabla ya kuanza mafunzo.
Utaratibu wa Kujiunga na JKT kwa Mwaka 2024
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, usajili wa kujiunga na mafunzo ya kujitolea utaanza rasmi tarehe 1 Oktoba, 2024.
Utaratibu wa maombi na usaili utaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini, ambapo vijana watatakiwa kuomba kupitia maeneo wanakoishi. Vijana waliochaguliwa watahitajika kuripoti katika makambi ya JKT kati ya tarehe 1 Novemba hadi 3 Novemba, 2024.
Kwa vijana wote ambao wanachukulia mafunzo haya kama fursa ya ajira, ni muhimu kuelewa kwamba JKT haitoi ajira wala kuwatafutia ajira kwenye taasisi au mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali. Badala yake, JKT inatoa mafunzo yatakayowasaidia vijana kujiajiri wenyewe baada ya kumaliza mafunzo haya ya JKT.
Sifa za Kujiunga na JKT 2024, Mafunzo ya Kujitolea
Ili kujiunga na JKT kwa kujitolea mwaka 2024, mwombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Raia wa Tanzania: Mwombaji lazima awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Umri: Umri wa mwombaji hutegemea kiwango cha elimu alichomaliza:
- Darasa la Saba: Umri wa miaka 16 hadi 18.
- Kidato cha Nne: Umri usizidi miaka 20.
- Kidato cha Sita: Umri usizidi miaka 22.
- Stashahada: Umri usizidi miaka 25.
- Shahada: Umri usizidi miaka 26.
- Shahada ya Uzamili: Umri usizidi miaka 27.
- Afya: Mwombaji anapaswa kuwa na afya njema na akili timamu. Pia, asiwe na alama yoyote ya michoro mwilini (tattoo).
- Tabia: Mwombaji anatakiwa kuwa na tabia njema, asiwe amewahi kupatikana na hatia mahakamani wala hajawahi kufungwa jela.
- Nyaraka Muhimu: Mwombaji anapaswa kuwa na:
- Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
- Cheti halisi cha kuzaliwa.
- Vyeti vya elimu halisi kwa wale waliohitimu Darasa la Saba, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Stashahada, Shahada au Shahada ya Uzamili.
- Masharti Mengine: Mwombaji asiwe amewahi kutumikia katika vyombo vya ulinzi kama Jeshi la Polisi, Magereza, au idara nyingine za serikali, na pia asiwe ameshiriki katika operesheni za awali za JKT kwa kujitolea au Mujibu wa Sheria.
- Matumizi ya Madawa ya Kulevya: Mwombaji asiwe amewahi kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi au vitu vingine haramu vinavyofanana na hayo.
Mwombaji atakayebainika kuwa na nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua kali za kisheria kulingana na taratibu zilizopo.
Vifaa Muhimu vya Kujiunga na JKT
Vijana wanaojiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea wanatakiwa kuwa na vifaa maalum kwa ajili ya mafunzo, ambavyo ni pamoja na:
- Bukta ya rangi ya bluu iliyokolea (dark blue) yenye mpira kiunoni, na mfuko mmoja nyuma, isiyo na zipu.
- Raba za michezo zenye rangi ya kijani au bluu.
- Shuka mbili za rangi ya blue bahari za kulalia.
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi kwa wale watakaopangwa kwenye mikoa yenye hali ya hewa ya baridi.
- Truck suit ya rangi ya kijani au bluu.
- Fulana ya kijani kibichi yenye kola ya duara isiyo na maandishi.
- Nauli ya kwenda na kurudi nyumbani kutoka makambini.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti