Kikosi cha Simba vs Fountain Gate Leo 15/04/2026
Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo watashuka dimbani kuwakabili wenyeji wao Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao utatimua vumbi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha saa 4:00 pm. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikisaka pointi muhimu.
Kikosi cha Simba vs Fountain Gate Leo 15/04/2026 kinaendelea kusubiriwa na mashabiki kuelekea mchezo huu wa Ligi Kuu ya NBC. Hadi sasa, vikosi rasmi vya kuanza mchezo havijawekwa wazi, huku kila timu ikiendelea na maandalizi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani. Vikosi rasmi vinatarajiwa kutangazwa saa moja kabla ya mchezo kuanza ambapo hapa tutakuletea vikosi hivyo mara tu vitakapo wekwa wazi
Hiki Apa Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Fountain Gate
Starting XI:
- Kassali (39)
- Duchu (15)
- Kibabage (32)
- Toure (25)
- De Reuck (C) (23)
- Kante (8)
- Gueye (7)
- Neo (35)
- Mwalimu (40)
- Chama (17)
- Oura (20)
Subs: Abel, Mligo, Vedastus, Mbegu, Semfuko, Mpanzu, Inno, Baraka, Morice & Chasambi
Simba yaingia na mwendelezo wa matokeo mazuri
Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika hali nzuri baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji uliowapa tiketi ya kufuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB. Matokeo hayo yanaipa timu hiyo hali ya kujiamini kuelekea mchezo huu.
Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, alisema timu yake imejiandaa vizuri kimwili na kimbinu kwa ajili ya mchezo huo, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza matokeo mazuri.
Alisema: “Tumewaandaa wachezaji vizuri kimwili na kimbinu, mechi iliyopita tulionesha hali ya kusaka ushindi na jambo la faida ni kuendelea kupata matokeo mazuri mfululizo.”
Simba pia inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate katika duru la kwanza ya ligi.
Fountain Gate yaanza enzi mpya chini ya Minziro
Kwa upande wa Fountain Gate, mchezo huu unakuwa wa kwanza kwa Kocha Mkuu Fred Felix ‘Minziro’ tangu atambulishwe Aprili 10, 2026 pamoja na msaidizi wake Mathias Wandiba, wakichukua nafasi ya Mohamed Ismail ‘Laizer’.
Minziro anaingia kwenye mchezo huu baada ya kuishuhudia timu hiyo ikipoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Azam katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB. Hivyo, mchezo huu unakuwa na uzito mkubwa kwa benchi hilo jipya la ufundi.
Meneja wa timu hiyo, Elias Zamkufo, alisema wanatambua ubora wa Simba lakini wanaamini uzoefu wa benchi la ufundi unaweza kuwasaidia kupata matokeo chanya.
Alisema: “Tunajua Simba ni timu kubwa na ukifanya makosa wanakuadhibu, hatupaswi kumdhibiti mchezaji mmoja bali kuwakabili wote, tunashukuru Kocha wetu anao uzoefu na ushindani kwenye soka.
“Mbinu zake zinaweza kutupa kitu, kimsingi tuko tayari kwa ajili ya mchezo huo ili kupata pointi tatu ambazo zitatupandisha nafasi nzuri kwenye msimamo, mashabiki waje kwa wingi kutusapoti.”
Aidha, alibainisha kuwa wachezaji wote wako fiti kwa ajili ya mchezo huo, huku waliokuwa majeruhi Daniel Joram na Ibrahim Parapanda wakirejea kikosini.
Tahadhari ya benchi la ufundi
Kocha msaidizi wa Fountain Gate, Mathias Wandiba, alisema timu inaingia kwenye mchezo huo kwa tahadhari, ikitambua ubora wa wapinzani wao. Alieleza kuwa maandalizi yao yamejikita zaidi katika kuwajenga kisaikolojia wachezaji kutokana na muda mfupi waliokuwa nao.
Wandiba alisema: “Hatujaweka ufundi mwingi kwakuwa ni muda mfupi lakini zaidi tumewaandaa kisaikolojia wachezaji wakapambane uwanjani, dhamira yetu ni timu ishinde ili tujinasue huko chini na tusishuke daraja.”
Msimamo wa ligi kabla ya mchezo
Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36, ikiachwa kwa pointi nane na Yanga waliopo kileleni. Fountain Gate inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 16 baada ya timu zote kucheza mechi 17.
Tofauti hiyo ya msimamo inaongeza uzito wa mchezo huu, huku kila timu ikiwa na malengo yake mahsusi kuelekea dakika 90 za mchezo.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply