Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 Morocco
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa orodha rasmi ya wachezaji walioteuliwa na kocha wa Timu ya Taifa ya wanaume, Miguel Gamondi, kuunda kikosi cha awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 zinazotarajiwa kufanyika Morocco.
Orodha hii imejumuisha wachezaji wanaocheza ndani na nje ya nchi, ikiwemo nyota wenye uzoefu mkubwa, vijana wapya wenye uwezo wa kuongeza ushindani, pamoja na wanandinga wanaoendelea kung’ara katika klabu zao za ndani na nje ya Tanzania.
Taarifa ya TFF imebainisha kuwa hatua ya awali ya kambi inalenga kufanya tathmini ya kiufundi na kuboresha uimara wa timu kabla ya kutangazwa kwa kikosi cha mwisho kitakachoshiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Gamondi ameita wachezaji wanaocheza ligi za ndani na wale wanaopata nafasi kwenye ligi za Ulaya, Asia na Amerika, jambo linaloonyesha dhamira ya kujenga timu shindani yenye mchanganyiko wa uzoefu na vipaji vipya.
Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025
- Hussein Masalanga – Singida Black Star
- Yakoub Suleiman – Simba SC
- Yona Amosi – Pamba Jiji FC
- Zuberi Foba – Azam FC
- Haji Mnoga – Salford City, England
- Iddi Selemani – Azam FC
- Ibrahim Abdulla – Young Africans
- Dickson Job – Young Africans
- Feisal Salum – Azam FC
- Cyprian Kachwele – Whitecaps FC, Canada
- Ahmed Pipino – KMC FC
- Abdul Suleiman – Azam FC
- Mbwana Samatta – Le Havre AC, France
- Morice Abraham – Simba SC
- Pascal Msindo – Azam FC
- Wilson Nangu – Simba SC
- Mohamed Hussein – Young Africans
- Lusajo Mwaikenda – Azam FC
- Mukrim Abdallah – Singida Black Star
- Nassor Saadun – Azam FC
- Elias Lawi – Azam FC
- Yusuph Kagoma – Simba SC
- Shomari Kapombe – Simba SC
- Mudahthir Yahya – Young Africans
- Saimon Msuva – Al-Talaba SC, Iraq
- Athumani Makambo – Coastal Union
- Vedastus Masinde – Simba SC
- Bakari Mwamnyeto – Young Africans
- Novatus Miroshi – Göztepe FC, Turkey
- Tarryn Allarakhia – Rochdale AFC, England
- Charles M’mombwa – Floriana FC, Malta
- Iddi Kipagwile – Dodoma Jiji
- Vitalis Mayanga – Mbeya City
- Khalid Habibu – Singida Black Star
- Edwin Balua – En Paralimniou, Cyprus
- Miano Danilo – FK Panevezys, Lithuania
- Alphone Mabula – FC Shamakhi, Azerbaijan
- Abdulkari Kiswanya – Namungo FC
- Abdulmalik Zakaria – Mashujaa FC
- Nathaniel Chilambo – Azam FC
- Said Khamis – Immigration FC, Malaysia
- Suleiman Mwalimu – Simba Sports Club
- Yahya Zaydi – Azam FC
- Offen Chikola – Young Africans
- Jackson Kasanzu – Tormenta FC, USA
- Ben Dismas – Simba SC
- Israel Mwenda – Young Africans
- Kelvin John – Aalborg BK, Denmark
- Kelvin Njoshi – Pamba Jiji FC
- Sabri Kondo – BK Häcken, Sweden
- Nickson Kibabage – Singida Black Star
- Paul Peter – JKT Tanzania
- Abel Josiah – JKT Tanzania U20
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo Wa Championship Ligi Daraja la Kwanza Tanzania 2025/2026
- Msimamo wa Kundi la Azam Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
- Simba Yachezea Kichapo cha Pili Mfululizo Makundi Klabu Bingwa
- Singida BS Yapata Pointi ya Kwanza Makundi Kombe la Shirikisho CAF
- Matokeo ya Stade Malien vs Simba leo 30/11/2025
- Kikosi cha Simba vs Stade Malien leo 30/11/2025
- Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 30/11/2025









Leave a Reply