Kikosi cha Yanga VS Fountain Gate Leo 04/12/2025
Kikosi cha Yanga leo kitashuka dimbani kuwakabili wageni wao Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex majira ya saa 10:00 jioni. Hii ni mechi muhimu kwa mabingwa hao watetezi ambao wamerejea kutoka majukumu ya kimataifa wakiwa na morali na mwenendo unaoendelea kupanda, wakati wapinzani wao wanahitaji matokeo ya kurejesha uhai baada ya safari ngumu kwenye michezo yao ya hivi karibuni.
Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kasi ya ushindani iliyoonekana katika mashindano yote waliyocheza msimu huu. Ubora wao umeonekana katika kila eneo la uwanja, hali iliyoendelezwa tangu kuanza kwa ligi. Wakati huo huo, Fountain Gate inarejea baada ya kichapo cha bao 2–0 dhidi ya JKT Tanzania, matokeo yaliyoonyesha changamoto wanazokutana nazo katika mechi muhimu.
Ukiangalia rekodi za timu hizi katika michezo ya karibuni, Yanga ina kumbukumbu nzuri dhidi ya Fountain Gate. Mchezo wao wa mwisho uliisha kwa Yanga kushinda mabao 4–0, huku msimu uliopita wakipata jumla ya mabao 9–0 katika mechi mbili za ligi. Hata hivyo, wafungaji wote wa ushindi huo wa 4–0 hawatakuwepo leo kutokana na majeraha na sababu za usajili ikiwamo Clement Mzize aliyeumia, pamoja na Stephanie Aziz Ki na Clatous Chama waliojiunga na timu nyingine.
Nguvu ya Yanga na Ubora wa Mfumo wao
Kikosi cha Yanga kimeendelea kujengeka katika misingi ya kasi, nidhamu na umiliki wa mpira kupitia mtindo wa kupiga pasi fupi. Timu imekuwa ikianzisha mashambulizi kutoka nyuma kwa utulivu kabla ya kupandisha kasi kupitia viungo wao wabunifu kama Maxi Nzengeli, Duke Abuya na Celestine Ecua.
Safu yao ya ulinzi imekuwa ngome imara msimu huu. Wakiongozwa na Dickson Job, Ibrahim Bacca na Bakari Mwamnyeto, Yanga imekuwa ikionesha mawasiliano mazuri na umakini wa hali ya juu. Katika mechi tatu zilizopita, wametoa nafasi chache sana kwa wapinzani na kuruhusu bao moja pekee, huku wakipachika jumla ya mabao tisa.
Katika maeneo ya pembeni, Yanga imekuwa ikiwatengenezea wapinzani wakati mgumu kutokana na matumizi bora ya fursa zinapopatikana katika maeneo ya kando ya uwanja — eneo ambalo Fountain Gate imeonekana kuwa na udhaifu.
Kocha Pedro Gonçalves alisisitiza kuwa licha ya ratiba ngumu iliyowachosha, bado dhamira ya kupata pointi tatu ipo pale pale. Alisema:
“Diarra (Djigui) na Pacome (Zouzoua) hawako sawa kiafya, lakini tunaamini waliopo wana uwezo wa kufanya vyema kwenye mechi iliyopo mbele yetu. Tutakwenda kutengeneza nafasi na kuzifanyia kazi, lakini kuhakikisha haturudii makosa tuliyofanya kwenye mechi zilizopita.”
Hali ya Fountain Gate Kabla ya Mchezo
Kwa upande wa Fountain Gate, changamoto imekuwa kukosa uzoefu dhidi ya timu kubwa. Timu imekuwa ikipoteza mipira kirahisi katikati ya uwanja na mara nyingi kushindwa kudhibiti presha ndani ya eneo lao la hatari, jambo linalowapa wapinzani nafasi nyingi za kutengeneza mabao.
Katika michezo tisa ya ligi waliyocheza mpaka sasa, Fountain Gate imeshinda mitatu, sare moja na kupoteza mitano. Wamefunga mabao manne pekee na kuruhusu mabao kumi, rekodi inayoonyesha mapungufu makubwa katika ufungaji na ulinzi.
Kocha wao Mohamed Ismail ‘Laizer’ alisisitiza kuwa wanatarajia mchezo wenye ushindani, akisema:
“Mchezo ujao dhidi ya Yanga hautakuwa mgumu kwetu wala mrahisi kwa wapinzani wetu kwa kuwa tumejipanga kutoa ushindani mkubwa. Najua wametoka kucheza kimataifa hivyo wako vizuri.”
Kikosi cha Yanga VS Fountain Gate Leo 21/04/2025
Kikosi rasmi cha Yanga kitakachoanza leo dhidi ya Fountain Gate kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9 alasiri. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Miloud Hamdi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
- Yanga VS Fountain Gate Leo 04/12/2025 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu NBC Leo 04/12/2025
- Simba vs Mbeya City Leo 04/12/2025 Saa Ngapi?
- TFF Yatangaza Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 Morocco
- Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026
- Msimamo Wa Championship Ligi Daraja la Kwanza Tanzania 2025/2026









Leave a Reply