Makundi ya Dar Port Kagame CECAFA Cup 2024 | Makundi ya CECAFA Kagame Cup 2024
Michuano ya CECAFA ambayo kwa sasa imepewa jina la CECAFA Dar Port Kagame Cup 2024 imerudi kwa kishindo, na klabu bingwa 12 za ukanda zimekusanyika Dar es Salaam, Tanzania, kuanza rasmi safari za kumsaka bingwa wa Afrika mashariki na kazi. Michuano hii imeanza kutimua vumbi tarehe 9 na mashabiki wa soka wataweza kuangalia klabu zao zikipambania kombe hili hadi 21 Julai. Je, ni nani atafuata nyayo za vigogo kama Simba SC na AFC Leopards waliotwaa taji hili mara sita kila mmoja?
Makundi ya Dar Port Kagame CECAFA Cup 2024
Kundi A: Coastal Union (Tanzania), Al Wadi (Sudan), JKU SC (Zanzibar), Dekedaha (Somalia)
Kundi A linaanza na wenyeji Coastal Union, ambao wana matumaini ya kutumia uwanja wa nyumbani kama faida. Al Wadi kutoka Sudan na JKU SC ya Zanzibar wana rekodi za kuheshimika, huku Dekedaha kutoka Somalia ikiwa ni timu changa yenye kiu ya kujitambulisha.
Kundi B: Al Hilal (Sudan), Gor Mahia (Kenya), Red Arrows (Zambia), Djibouti Telecom (Djibouti)
Kundi B ni kundi la kifo lenye timu zenye majina makubwa. Al Hilal kutoka Sudan ni wababe wa soka la Afrika, huku Gor Mahia kutoka Kenya wakirejea dimbani wakiongozwa na kocha mpya Mbrazil, Leonardo Martins Neiva. Red Arrows kutoka Zambia, mabingwa wa ligi yao, ni wageni wenye hatari kubwa. Djibouti Telecom, ingawa hawana uzoefu mwingi, wanaweza kuwa nguvu ya kushangaza.
Kundi C: SC Villa (Uganda), APR FC (Rwanda), Singida Black Stars (Tanzania), El Merriekh Bentiu (Sudan Kusini)
Kundi C lina mabingwa wa hivi karibuni wa Uganda, SC Villa, ambao walivunja ukame wa miaka 20. APR FC ya Rwanda, wakiongozwa na kocha Darko Novic, wanalenga kuonyesha ubora wao katika ukanda huu. Singida Black Stars, timu inayokua kwa kasi Tanzania, ina kiu ya kuonyesha uwezo wake. El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini inaleta changamoto kutoka nchi jirani.
Mapendekezo ya mhariri:
Weka Komenti