Namungo FC vs Yanga Sc Leo 22/02/2026 Saa Ngapi?
Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 inaendelea kushika kasi leo katika viwanja tofauti nchini huku kila timu ikiingia dimbani kwa lengo la kukusanya pointi tatu muhimu katika mbio za kujiimarisha kwenye msimamo. Katika ratiba ya leo, macho na masikio ya mashabiki wengi yataelekezwa Lindi kwenye pambano la kukatana shoka kati ya Namungo FC na Young Africans SC.
Namungo FC vs Yanga Sc Leo 22/02/2026 Saa Ngapi?
Kwa mujibu wa ratiba ya leo, mchezo kati ya Namungo FC vs Yanga Sc Leo utapigwa kuanzia majira ya saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Majaliwa, Mkoani Lindi. Huu ni moja ya mechi zinazotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, hasa kwa kuzingatia nafasi za timu hizi kwenye msimamo wa ligi na rekodi zao za michezo iliyopita wanapokutana.
Rekodi ya Namungo dhidi ya Yanga
Yanga, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wanaingia katika mchezo huu wakiwa na historia nzuri dhidi ya Namungo. Tangu msimu wa 2020/2021, timu hizo zimekutana mara 12 kwenye Ligi Kuu:
- Yanga imeshinda mechi saba mfululizo
- Sare zimekuwa tano
- Namungo haijapata ushindi
Takwimu hizo zinaipa Yanga hali ya kujiamini kabla ya kushuka dimbani, lakini soka hubeba matokeo yasiyotabirika, hasa pale timu ya nyumbani inapocheza mbele ya mashabiki wake.
Msimamo wa Ligi Kabla ya Mchezo
Kuelekea kwenye mchezo wa leo:
- Namungo ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 14 (imeshinda tano, sare tano na kupoteza nne).
- Yanga ina pointi 22 ikiwa imecheza mechi nane.
Ushindi kwa Namungo utaiwezesha kufikisha pointi 23 na kuishusha Yanga kwenye msimamo. Hili linaifanya mechi ya leo kuwa na uzito mkubwa kwa pande zote mbili.
Kwa upande wa mabingwa watetezi Yanga, ushindi utaiwezesha kuendelea kujiimarisha katika nafasi za juu na kuongeza kasi katika kuhakikisha ubingwa unabaki mikononi mwao huku ikidumisha rekodi yake nzuri dhidi ya wapinzani hao.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mbio za Ubingwa EPL Zapamba Moto Baada ya Arsenal Kudondosha Pointi Dhidi ya Wolves
- Barcelona Yatakiwa Kulipa Pauni 26M Kumng’oa Rashford Manchester United
- Serikali Yaidhinisha Rasmi Marekebisho ya Katiba ya Simba SC Kupitia BMT
- Benfica vs Real Madrid Yasimama Kwa Dakika 10 Kufuatia Tuhuma za Ubaguzi wa Rangi kwa Vinicius Jr









Leave a Reply