Yaliyomo: Cv Ya Steven Mukwala Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025 | wasifa wa Steven Mukwala | Orodha ya Timu Alizochezea Steven Mukwala kabla ya kujiunga na Simba Sc 2024/2025
Klabu ya Simba SC imethibitisha rasmi leo Julai 2 kumsajili Steven Mukwala kutoka Klabu ya Asante Kotoko ya Nchini Ghana.
Huu ni usajili wa tatu kufanywa na Simba SC baada ya ule wa Lameck Lawi na Joshua Mutale ambao wanatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi cha Simba kuelekea msimu wa 2024/2025.
Steven Mukwala, ambaye ni mshambuliaji mahiri na mwenye kipaji kikubwa cha kusakata boli, anatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba SC ambayo ilionekana kuwa butu msimu wa 2023/2024.
Usajili huu unakuja wakati ambapo Simba SC inajiandaa kwa msimu mpya wa ligi na michuano ya kimataifa ya CAF confederation cup, huku ikilenga kuimarisha kikosi chake na kuhakikisha mafanikio makubwa. Mukwala, mwenye uzoefu mkubwa katika ligi mbalimbali, anatarajiwa kuwa mchezaji muhimu na tegemeo katika safari ya Simba SC kuelekea ubingwa.
Katika makala hii, tutachambua kwa kina wasifu wa Steven Mukwala, kuanzia maisha yake ya awali, safari yake ya soka, takwimu na rekodi zake, hadi jinsi anavyotarajiwa kuathiri kikosi cha Simba SC na matarajio yake ya baadaye.
Cv Ya Steven Mukwala Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025
Kipengele | Maelezo |
Jina Kamili | Steven Dese Mukwala |
Tarehe ya Kuzaliwa / Umri | Julai 15, 1999 (Miaka 24) |
Mahali pa Kuzaliwa | Makindye, Uganda |
Urefu | 1.76 m |
Uraia | Uganda |
Nafasi | Mshambuliaji – Centre-Forward |
Klabu ya Sasa | Simba SC |
Amejiunga | Julai 2, 2024 |
Safari ya Soka ya Steven Mukwala
Steven Mukwala ameonesha kiwango bora cha soka tangu aanze safari yake ya soka la kulipwa na kufanikiwa kukamilisha sajili mbalimbali katika timu tofauti. Hapa chini ni historia ya uhamisho wa Steven Mukwala:
Msimu | Tarehe | Alipotoka | Aliyejiunga | Aina ya Uhamisho |
24/25 | Julai 2, 2024 | Asante Kotoko | Simba Sc | – |
22/23 | Agosti 3, 2022 | URA FC | Asante Kotoko | – |
20/21 | Oktoba 27, 2020 | Vipers SC | URA FC | – |
19/20 | Juni 30, 2020 | Maroons FC | Vipers SC | Mwisho wa Mkopo |
19/20 | Julai 1, 2019 | Vipers SC | Maroons FC | Mkopo |
17/18 | Julai 1, 2017 | Haijulikani | Vipers SC | – |
Timu Alizochezea Steven Mukwala
- URA FC: Steven Mukwala alijiunga na URA FC mara mbili katika safari yake ya soka. Mara ya kwanza alitokea Vipers SC mnamo Oktoba 27, 2020, na mara ya pili alitoka Asante Kotoko mnamo Agosti 3, 2022.
- Vipers SC: Mukwala alijiunga na Vipers SC mnamo Julai 1, 2017. Akiwa na Vipers SC, aliwahi kwenda kwa mkopo Maroons FC mnamo Julai 1, 2019. Baada ya msimu mmoja wa mkopo, alirudi Vipers SC mnamo Juni 30, 2020.
- Maroons FC: Akiwa Maroons FC kwa mkopo kutoka Vipers SC, Mukwala alifanikiwa kucheza vizuri na kupata uzoefu muhimu ambao ulimsaidia baada ya kurejea Vipers SC.
- Asante Kotoko: Uhamisho wake wa hivi karibuni ulikuwa kutoka URA FC kwenda Asante Kotoko mnamo Agosti 3, 2022. Akiwa Asante Kotoko, Mukwala aliendelea kuonyesha uwezo wake mkubwa kama mshambuliaji hodari.
- Simba SC: Mnamo Julai 2, 2024, Steven Mukwala alijiunga rasmi na Simba SC, akitarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kwa msimu wa 2024/2025.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba
- Azam Yatuma Ofa Kwa Simba Kumsajili Kipa Aishi Manula
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Wachezaji Wapya Simba 2024/2025
- Simba Day 2024: Tarehe Rasmi Yatangazwa na Simba SC
- Mishahara Ya Wachezaji Wa Simba 2024/2025
- Wachezaji walioachwa na Simba 2024/2025
- Kikosi Cha Simba 2024/2025 | Wachezaji Wote wa Simba
Weka Komenti