Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 15/04/2026

Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 15/04/2026

Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 15/04/2026 inaendelea leo Jumatano kwa michezo miwili muhimu inayohusisha timu zinazopambania malengo tofauti kwenye msimamo wa ligi. Mashabiki wanatarajia kufuatilia kwa karibu michezo hii ambayo itarushwa mubashara kupitia AzamSports1HD.

Ratiba rasmi ya mechi za Ligi Kuu NBC leo Aprili 15, 2026 imeainishwa hapa chini, ikionyesha muda na viwanja vya kila mchezo kwa urahisi wa ufuatiliaji.

Fountain Gate vs Simba SC

  • Muda: Saa 10:00 jioni
  • Uwanja: Sheikh Amri Abeid

Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 15/04/2026

Coastal Union vs Dodoma Jiji

  • Muda: Saa 12:30 jioni
  • Uwanja: Mkwakwani

Katika mchezo wa Fountain Gate dhidi ya Simba, macho yote yatakuwa kwa kocha mpya Fred Felix ‘Minziro’ ambaye anaanza rasmi majukumu yake baada ya kutambulishwa Aprili 10, 2026. Akiwa jukwaani hivi karibuni, aliishuhudia timu yake ikipoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Azam katika Kombe la Shirikisho la CRDB, wakati Simba wakishinda 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji na kufuzu robo fainali.

Meneja wa Fountain Gate, Elias Zamkufo, alisema wanaelewa ugumu wa mchezo huo lakini wana imani na uzoefu wa benchi la ufundi. Alibainisha kuwa wachezaji wote wako fiti, huku Daniel Joram na Ibrahim Parapanda wakirejea kutoka majeruhi. Alisisitiza umuhimu wa kucheza kama timu dhidi ya Simba.

Kocha msaidizi Mathias Wandiba alieleza kuwa maandalizi yamejikita zaidi katika kuwaandaa kisaikolojia wachezaji kutokana na muda mfupi waliokuwa nao, akisisitiza kuwa lengo ni kupata ushindi ili kujinasua kwenye nafasi za chini.

Kwa upande wa Simba, kocha mkuu Steve Barker alisema kikosi chake kipo tayari kimwili na kimbinu, kikilenga kuendeleza matokeo mazuri. Simba pia ina kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate katika duru la kwanza.

Kwa sasa, Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 36, nyuma ya Yanga kwa pointi nane, wakati Fountain Gate ipo nafasi ya 14 na pointi 16 baada ya mechi 17 kwa kila timu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio Mechi ya Fountain Gate vs Simba 15/04/2026
  2. Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Bank Federation Cup 2025/2026
  3. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026
  4. Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 11/04/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo