Matokeo ya Yanga vs Mbeya City Leo 16/04/2026

Matokeo ya Yanga vs Mbeya City Leo 16/04/2026

Kikosi cha Yanga leo kinashuka dimbani kuikabili Mbeya City katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex majira ya saa 12:30 jioni, huku macho ya mashabiki wengi yakielekezwa kuona namna mabingwa hao watetezi watakavyotumia faida ya uwanja wa nyumbani kusaka alama tatu muhimu.

Mchezo huu unakuja wakati Yanga ikiwa katika kiwango bora na ikisaka kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza, sambamba na kurejea kwa nyota wake muhimu waliokuwa nje, hali inayoongeza nguvu na matarajio makubwa kuelekea pambano hilo dhidi ya Mbeya City ambayo nayo imejiandaa kupambana kwa umakini mkubwa.

Matokeo ya Yanga vs Mbeya City Leo 16/04/2026

Matokeo ya Mechi (Live Updates)

Yanga SC vs Mbeya City
📅 16/04/2026
⏰ Saa 12:30 Jioni
🏟️ KMC Complex

Yanga Sc VS Mbeya City

Kikosi cha Yanga kinaingia kwenye mchezo huo kikiwa na nguvu mpya kufuatia kurejea kwa kipa namba moja Djigui Diarra, ambaye amemaliza adhabu ya kusimamishwa mechi tatu.

Kocha Pedro Goncalves alithibitisha umuhimu wa kurejea kwake akisema:

“Ni taarifa njema kwetu, Diarra ni mchezaji muhimu na kiongozi uwanjani.”

Aidha, mshambuliaji Prince Dube naye amerejea baada ya kuuguza majeraha ya misuli na anatarajiwa kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga katika mchezo wa leo.

Hata hivyo, Laurindo Aurellio ‘Depu’ bado hajaweza kurejea kikosini, huku Emmanuel Mwanengo naye akikosekana kutokana na majeraha.

Rekodi na Malengo ya Yanga

Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa kwenye mwendelezo mzuri wa kutopoteza mechi 38 za ligi mfululizo, na inalenga kuendeleza rekodi hiyo muhimu.

Katika mechi 12 zilizosalia, mabingwa hao watetezi wanahitaji matokeo mazuri ili:

Kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo
Kumaliza msimu bila kupoteza
Kufikia rekodi ya mechi 49 bila kupoteza

Kocha Pedro alisisitiza:

“Tunauhitaji mkubwa wa alama tatu, lakini lazima tuwe na umakini mkubwa.”

Mbeya City Wajipanga Kuzuia Presha

Kwa upande wa Mbeya City, kocha Mecky Maxime amesema timu yake ipo tayari kwa mchezo huo mgumu dhidi ya vinara wa ligi.

Alieleza:

“Ni mechi ngumu, lazima tuingie kwa umakini na kuwaheshimu Yanga.”

Mbeya City inaingia ikiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya Yanga msimu huu baada ya kulazimisha sare ya 0-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Mbeya.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 16/04/2026
  2. Matokeo ya Fountain Gate vs Simba Leo 15/04/2026
  3. Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Bank Federation Cup 2025/2026
  4. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo