Kikosi cha Yanga vs Mbeya City Leo 16/04/2026

Kikosi cha Yanga vs Mbeya City Leo 16/04/2026

Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kushuka dimbani kuvaana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, huku mashabiki wakisubiri kuona mabadiliko ya kikosi kufuatia kurejea kwa baadhi ya nyota muhimu waliokuwa nje kwa sababu mbalimbali.

Mchezo huo wa leo Alhamisi, Aprili 16, 2026, utaanza majira ya saa 12:30 jioni, ukiwa ni moja ya mechi zinazovuta hisia kubwa kutokana na ushindani uliopo kati ya timu hizo mbili.

Taarifa Muhimu za Mechi

  • Mechi: Yanga SC vs Mbeya City
  • Tarehe: 16 Aprili 2026
  • Uwanja: KMC Complex
  • Muda: Saa 12:30 jioni

Kikosi cha Yanga vs Mbeya City Leo 16/04/2026

Hiki Apa Kikosi cha Yanga Kilichotangazwa Leo dhidi Mbeya City Leo 16/04/2026

  • 28 MASALANGA
  • 33 MWENDA
  • 15 HUSSEIN
  • 3 MWAMNYETO
  • 4 BACCA
  • 28 ABUYA
  • 7 MAXI
  • 27 MUDATHIR
  • 29 DUBE
  • 10 PACOME
  • 20 OKELLO

Wachezaji wa ziada: Semsey, Yao, Boka, Assink, Abubakar, Abdulnasir, Sheikham, Andabwile, Damaro, Edmund

Habari Njema Kikosi cha Yanga

Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, amepata nafuu kubwa kuelekea mchezo wa leo baada ya kurejea kwa kipa namba moja, Djigui Diarra, aliyemaliza adhabu ya kusimamishwa mechi tatu. Adhabu hiyo ilitokana na tukio la kinidhamu katika mchezo wa awali dhidi ya Mtibwa Sugar. Akizungumza kuelekea mchezo huo, Pedro alieleza umuhimu wa kurejea kwa Diarra akisema:

“Ndiyo Diarra amerudi, ni taarifa njema. Ni mchezaji muhimu na kiongozi uwanjani, tunafurahia kurejea kwake.”

Kurejea kwa kipa huyo kunakuja wakati ambao kipa mwingine, Aboutwalib Mshery, bado anakabiliwa na majeraha ya goti, hali iliyosababisha timu kutegemea chaguo mbadala katika mechi zilizopita.

Dube Aongeza Nguvu Safu ya Ushambuliaji

Mbali na Diarra, mshambuliaji Prince Dube pia amerejea kikosini baada ya kukosa michezo kadhaa kutokana na majeraha ya misuli. Katika mchezo uliopita dhidi ya Pamba Jiji, Dube alipata dakika 14 tu, lakini leo anaweza kuanza kikosi cha kwanza.

Pedro alisisitiza mchango wa Dube katika safu ya ushambuliaji:

“Ujio wake utaongeza nguvu na ufanisi kwenye eneo la ushambuliaji.”

Hata hivyo, mshambuliaji mwingine, Laurindo Aurellio ‘Depu’, bado hajawa fiti kurejea uwanjani, wakati Emmanuel Mwanengo naye anatarajiwa kuukosa mchezo huo kutokana na majeraha.

Yanga inaingia kwenye mchezo huu wa leo ikiwa na lengo la kuendeleza ubora wake na kusaka alama tatu muhimu ili kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi. Kocha Pedro alibainisha kuwa:

“Tunauhitaji mkubwa wa alama tatu, lakini lazima tuwe na tahadhari. Mbeya City ni timu nzuri yenye uzoefu.”

Kwa sasa, Yanga ipo kwenye mwendo mzuri ikiwa haijapoteza mechi 38 mfululizo za ligi, na inalenga kufikia rekodi ya mechi 49 bila kupoteza iliyowekwa misimu iliyopita.

Mbeya City Yajipanga Kwa Umakini

Kwa upande wa Mbeya City, Kocha Mecky Maxime amesema timu yake imejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo mgumu.

Alisema:

“Tunajua tunacheza na timu inayoongoza ligi. Mechi kama hizi zinahitaji umakini mkubwa na heshima kwa mpinzani.”

Mbeya City inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mmoja tu dhidi ya Yanga tangu mwaka 2016, huku ikipoteza mara nyingi zaidi katika rekodi ya mikutano yao.

Hata hivyo, Maxime alisisitiza kuwa historia si kigezo kikubwa katika soka:

“Mpira hauna historia, kinachotokea siku ya mechi ndicho kinaamua matokeo.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 16/04/2026
  2. Matokeo ya Fountain Gate vs Simba Leo 15/04/2026
  3. Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Bank Federation Cup 2025/2026
  4. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo