Gharama za Kukodi Uwanja wa KMC Complex | Bei ya Kukodisha uwanja wa KMC Mwenge
Uwanja wa KMC Complex, ulioko Mwenge, Dar es Salaam, umekuwa kivutio kikubwa kutokana na miundombinu yake ya kisasa na uwezo wake wa kuchukua mashabiki 8,000. Uwanja huu ni mali ya Manispaa ya Kinondoni na umejengwa kwa ushirikiano na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Ni uwanja unaotumiwa na klabu ya Kinondoni Municipal Council F.C almaharufu kwa jina la KMC FC kama uwanja wao wa nyumbani, lakini pia unakodishwa kwa vilabu vingine na shughuli mbalimbali za kijamii.
Katika msimu wa soka wa 2023/2024, vilabu vikubwa kama Simba SC na Yanga SC walikuwa miongoni mwa timu zilizotumia uwanja huu kwa ajili ya mechi zao za nyumbani, kutokana na matengenezo yaliyoendelea kwenye viwanja vingine jijini Dar es Salaam, ikiwemo Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Gharama za Kukodi Uwanja wa KMC Complex kwa Shughuli Mbalimbali
Kwa wale wanaotaka kukodi uwanja huu, gharama zimewekwa kulingana na aina ya shughuli na kiwango cha matumizi.
Daniel Madenyeka, meneja wa uwanja huo, amefafanua kwa kina gharama hizi, ambazo zinazingatia aina ya tukio, kama vile mechi za ligi kuu, mazoezi ya timu, au matumizi ya biashara kama vile kurekodi video au filamu.
1. Mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara
Uwanja wa KMC Complex unatozwa kiasi cha shilingi 6,000,000 kwa kila mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hii inajumuisha matumizi yote ya uwanja, ikiwa ni pamoja na usalama, usimamizi wa mchezo, na huduma zote zinazohitajika kuhakikisha mechi inafanyika kwa mafanikio. Gharama hii ni ya kawaida kwa vilabu vikubwa nchini, kama vile Simba SC na Yanga SC, ambao wamekuwa wakitumia uwanja huu kwa mechi zao wakati mwingine.
2. Mazoezi ya Timu
Kwa timu zinazohitaji kukodi uwanja kwa ajili ya mazoezi, gharama imewekwa kuwa shilingi 300,000 kwa kila mechi ya mazoezi.
Gharama hii inajumuisha matumizi ya miundombinu ya uwanja, kama vile vyumba vya kubadilishia nguo, eneo la kuchezea, na huduma nyinginezo muhimu kwa mazoezi ya timu.
3. Shughuli nyengine za Biashara (Shooting na Filamu)
Kwa watu au makampuni yanayopenda kutumia uwanja kwa shughuli za biashara kama vile kurekodi video au filamu (shooting), gharama ya kukodisha uwanja ni shilingi 200,000. Uwanja huu umevutia makampuni mengi ya burudani kutokana na ubora wa miundombinu yake, na unatumika mara kwa mara kwa ajili ya kurekodi matangazo ya biashara, filamu, na vipindi vya televisheni.
Umuhimu wa Uwanja wa KMC Complex katika Soka la Tanzania
Uwanja wa KMC Complex sio tu maskani ya timu ya KMC FC, bali pia ni sehemu muhimu katika maendeleo ya soka la Tanzania. Uwepo wa uwanja huu umeongeza chaguo la vilabu vya Tanzania, haswa kwa timu ambazo hazina viwanja vyao binafsi. Simba SC na Yanga SC, vilabu vikubwa zaidi nchini, mara kadhaa wamekuwa wakitumia uwanja huu katika mechi zao za nyumbani.
Uwanja huu una miundombinu ya kisasa inayojumuisha vyumba vya wachezaji, sehemu za mapumziko kwa waamuzi, na mfumo mzuri wa usalama ambao unahakikisha usalama wa wachezaji na mashabiki wakati wa mechi na shughuli nyinginezo.
Jinsi ya Kukodi Uwanja wa KMC Complex
Kwa wale wanaopenda kukodi uwanja wa KMC Complex kwa shughuli yoyote, iwe ni kwa mechi za ligi, mazoezi, au matumizi ya biashara, taratibu za kukodi uwanja ni rahisi. Unachohitajika kufanya ni kuwasiliana na menejimenti ya uwanja kwa njia ya simu au barua pepe na kufanya mawasiliano mapema ili kuhakikisha tarehe unayotaka inapatikana.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti