Hawa Apa Maofisa wa Mechi ya Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup 2024/2025

Maofisa wa Mechi ya Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup 2024/2025

Baada ya mechi mbili ngumu dhidi ya Simba SC katika Ligi Kuu Tanzania Bara, leo hii Singida Black Stars wanapata fursa ya kulipa kisasi katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank Federation Cup msimu wa 2024/2025. Pambano hili litapigwa katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati, mkoani Manyara, kuanzia saa 9:30 alasiri (15:30 EAT), Mei 31, 2025.

Ingawa uwanja huu umewekwa kama eneo la kati (neutral ground), jiografia ya eneo hilo inawapa faida ya karibu Singida BS, kwani ni umbali wa kilomita 150 hadi 180 kutoka Singida, ukilinganisha na Simba SC ambao wanatoka Dar es Salaam, umbali wa zaidi ya km 600.

Kwa Simba SC, hii ni mechi ya tatu mfululizo ndani ya wiki moja baada ya kutoka sare dhidi ya RS Berkane ya Morocco kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, na kisha kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Singida BS kwenye Ligi Kuu.

Kwa upande wa Singida, mechi hii inakuja siku nne tu baada ya kipigo hicho kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi, hivyo kuongeza hamasa ya kutafuta ushindi na kutinga fainali.

Maofisa Watakaosimamia Mechi ya Simba SC vs Singida BS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na CRDB Bank kama wadhamini wakuu, wametangaza orodha ya maofisa watakaosimamia mchezo huu wa pili wa nusu fainali. Orodha hii imeundwa kwa umakini ili kuhakikisha mchezo unachezwa kwa haki na kwa kufuata kanuni zote za mpira wa miguu.

Maofisa wa Mechi (Match Officials):

  • Refa Mkuu (REF): Ahmed Arajiga – Manyara
  • Msaidizi wa Kwanza (A1): Glory Tesha – Dar es Salaam
  • Msaidizi wa Pili (A2): Athuman Rajab – Kigoma
  • Rekodi na Taarifa (RR): Julius William – Manyara
  • Kamishna wa Mechi (MC): Isaack Munis – Kilimanjaro
  • Msimamizi wa Waamuzi (RA): Samwel Mpenzu – Arusha
  • Mratibu wa Uwanja (SC): Yohana Mkumbo – Manyara
  • Mratibu wa Usalama (SG): Shafi Mohamed – Manyara
  • Daktari wa Mechi (MD): Abubakar Mjaka – Manyara
  • Mratibu wa Vyombo vya Habari (BVM): Mussa Seif – Dar es Salaam
  • Msaidizi wa Sekretarieti (CS): Triphonia Temba – Manyara
  • Msambazaji wa Vifaa (COMP): Baraka Kizuguto – Dar es Salaam

Maofisa wa Mechi ya Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup 2024/2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025
  2. Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025 Saa Ngapi?
  3. Coastal Union Yapiga Hesabu Kali Kumchukua Anicet Kiazayidi
  4. Chelsea Yaipiga Bao Manchester United Usajili wa Liam Rory Delap
  5. Xabi Alonso Aahidi Kurejesha Ufalme wa Real Madrid
  6. Singida BS Yashindwa Kutamba Mbele ya Simba Ligi Kuu NBC
  7. Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 – Pakua PDF Hapa!
  8. Erik Ten Hag Atambulisha Rasmi Kama Kocha Mkuu Bayer Leverkusen
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo